Unawezaje kupata pesa au faida kwa kumiliki blogu?

Unataka kutenegeneza pesa kirahisi sio?, bila shaka, kila mtu anataka kutengeneza pesa halali imsaidie kusukuma maisha yake ya kila siku. Pengine umewahi sikia kuwa ukimiliki blogu ama tovuti unaweza kutengeneza pesa kirahisi?, ndio yawezekana kutengeneza pesa kirahisi kwa kutumia blogu, ila usiwe na shauku sana maana si rahisi tu. Wasomaji wangu wengi wamenitumia ujumbe na wengine kunipigia simu kuuliza nawezaje kupata pesa nikiwa na blogu yangu? Leo nitakushirikisha baadhi tu ya mbinu zinazotumika kupata pesa, na pia mambo muhimu unayopaswa kuyazingatia ili kufanikisha hilo.

Wengi wakiniuliza swali hili, huwa napata picha kwamba, wanahisi blogu ni kama kitu ambacho ukiwa nacho tu chenyewe kinafanya kazi hiyo ya kutengeza faida, na wengine hudhani, pengine walipotoshwa kuwa anaweza anzisha blogu na kuanza kupata pesa bila yeye kama mmiliki wa blogu kuweka juhudi zozote zile!, Hapana, tena ukiwa bloga mpya ndio inakuwa ni ngumu zaidi kupata faida, tazama orodha hii ndogo ya mambo ambayo unapaswa kufanya:

  1. Andaa na anzisha blogu yako
  2. Anza kuandaa na kuchapisha maudhui muhimu kwenye blogu yako
  3. Tafuta wasomaji na wafuatiliaji wa blogu yako
  4. Jenga mahusiano na ushiriki na wasomaji wa blogu yako
  5. Weka mifumo mbalimbali ya kupata pesa kupitia blogu yako

 

Unaona?, kupata pesa ni jambo la mwisho kabisa katika hatua hizo, ila kwa sababu ni hatua tano unaona ni kama rahisi sio?, nitazielezea zaidi hizo hatua ili upate kelewa juhudi unazotakiwa kuwekeza.

1. Andaa na anzisha blogu yako

Ndio, ni lazima uwe na blogu, na uwe unaimiliki wewe mwenyewe, inaweza kuwa rahisi kujifunza jinsi ya kuanzisha blogu kwa kusoma bandiko hili. ambalo ndilo limefanya niulizwe mswali mengi sana kuhusu faida.

2. Anza kuandaa na kuchapisha maudhui muhimu kwenye blogu yako

Blogu haina maana yeyote kama haina maudhui, maudhui(Content) ndio kitu pekee kitakacho tofautisha blogu yako na blogu zingine mtandaoni, maudhui ndio yatakayo kupatia wasomaji na wafuatiliaji wakudumu na hata wapya kwenye blogu yako.

Kimsingi hili ndio jambo la muhimu sana kuzingatia, mfano mwandishi wa habari ana nafasi nzuri ya kuwa na mudhui kwa sababu anakua na habari mpya kila mara, namna atakavyoziandaa habari zake na kuzichapisha kwa wakati inampa fursa kutumia blogu kuwafikia watu wengi kwa urahisi zaidi na wengi watapenda kuarifiwa punde tu unapochapisha habari mpya.

Chochote unachotaka kukizungumzia kwenye blogu yako chaweza kuwa ni kinalenga jamii fulani, au kundi fulani mfano watoto, vijana, wazee, wakulima, wanafunzi nakadhalika, jitahidi kiwe ni bora na chenye upekee. Maudhui mazuri na yenye muelekeo chanya yatawafanya wasomaji wako wajihisi kukufahamu na kukuamini sana hivyo kukuwekea mazingira bora zaidi ya kupata pesa baadae kupitia blogu yako.

3. Tafuta wasomaji na wafuatiliaji wa blogu yako

Blogu yako  ni mpya, hakuna mtu anaifahamu na unaamini una maudhui mazuri, sasa weka juhudi ya kuwapata wasomaji na wafuatiliaji, unatakiwa kuitangaza blogu yako. Muhimu hapa ni kujua ni watu gani (type of people) unaotaka wawe wasomaji na wafuatiliaji wa blogu yako. Kwa mfano umeandaa blogu ya mapishi!, ukishafahamu wasomaji wako ni watu wanaojihusisha na mambo ya mapishi basi fuatilia aina hii ya watu inaweza patikana wapi mtandaoni. Andaa orodha fupi yenye vitu kama:

  • Je!, wanafuatilia blogu zipi zingine zinazofanana au tofauti na maudhui ya blogu yako?
  • Wanashiriki kwenye majukwa gani mtandaoni? mfano (JamiiForums)
  • Kuna vipindi vya radio ama tv wanaweza kuwa wafuatilia pia?
  • Wanatumia mitandao ipi ya kijamii? orodhesha walau mitatu mikuu
  • Wanafuatlia watu gani kwenye hiyo mitandao ya kijamii?

 

Kwenye maeneo hayo utakayobainisha wasomaji unaowahitaji wanaweza kuwepo, wanaweza kuwa wanashiriki kwa kuchangia maoni na kulekezana. Hivyo na wewe inafaa uanze kuwa mshiriki wa maeneo hayo pia ili wakufahamu na pengine unaweza kutumia mwanya huo kuwajulisha na kuwakaribisha kuangalia blogu yako.

Muhimu ni kujenga uwepo wako, ufahamu, na kuchangia/kuongeza dhamani, epuka kuonekana kama mkorofi wa mtandaoni (spammy) kana kwamba unalazimisha watu wajue blogu yako tu, lakini wala huchangii mambo ya msingi wala kushauri.

Pia bila ushiriki wako, unaweza kuandaa bajeti ya matangazo na kutangaza blogu yako kwenye maeneo hayo ili ipate kufahamika.

4. Jenga mahusiano na ushiriki na wasomaji wa blogu yako

Kwa kuzingatia hizo hatua hapo juu, utakuwa na blogu nzuri, yenye maudhui sahihi na bila shaka umeanza kupata  wasomaji, sasa unapaswa kujenga mahusioano ya karibu na wasomaji wako ili waendelee kubaki na pia kukuletea wasomaji wapya.

Jibu maswali yao wanayouliza kuhusu mada husika kwa wingi kadri unavyoweza, pia wasiliana na baadhi yao wanapohitaji mawasiliano nawe kwa njia ya barua pepe nakadhalika.

Kushirikiana na wasomaji ni njia nzuri kukuwezesh akuapata pesa kupitia blogu yako.

5. Weka mifumo mbalimbali ya kupata pesa kupitia blogu yako

Sasa, umeshafanya yote yamsingi, lakini kupata pesa bado, na unahitaji kujaribu na kujuhudi njia mbalimbali kupata pesa. Bado safari ya kujifunza inaendelea, kuna njia nyingi sana za kupata pesa, ila hapa nitorodhesha chache ambazo mimi binafsi huwa nawashauri watu kuzitumia, tena ni njia ambazo bloga wengi huzitumia kupata pesa. Tuanze kujifunza njia hizi:

Kupata pesa kupitia matangazo ya CPC au CPM

Hii ni njia kuu ambayo hutumiwa sana na wamiliki blogu kupata pesa kwa kuweka matangazo madogo madogo kwenye kurasa za blogu zao, ziko aina mbili;

  • CPC/PPC – Cost per Click (au Pay Per Click), matanagazo ambayo yanakuwepo kwenye kurasa au pembeni mwa kurasa ya blogu yako yatakuingizia pesa kila msomaji atakapo gonga (click) tangazo hilo.
  • CPM – Cost per 1000 Impressions, yani kadiri tangazo litakavyoonekana mara nyingi katika nyakati tofauti tofauti na wasomaji tofauti tofauti utapata pesa kutoka kwa anayetangaza.

 

Google Adsense ndio mtandao maarufu wa kuchapisha na kupachika matangazo ya namna hii kwa wamiliki wa tovuti na blogu mbali mbali duniani, na inawalipa wamiliki wa blogu hizi vizuri kadiri blogu husika invyofaya vizuri kuzingatia hatua tulizojifunza awali, matangazo yanayopachikwa huteuliwa kielectroniki kuendana na maudhui, pia lugha ya blogu yako.

Uza matangazo binafsi

Ukiwa na watembeali wengi wa blogu yako kwa siku, sio lazima kutumia mitandao ya matangazo kama Google Adsense, Badala yake Makampuni yanaweza kukufuata moja kwa moja kutaka uwatangazie biashara zao. Unaweza pia kuwasiliana na wahusika moja kwa moja, na kwa kuwa hakuna mtu wa kati, hii inakuwezesha kuweka viwango unvyotaka kutoza kwa kila tangazo na ukapata faida kubwa zaidi.

Tangazo linaweza kuwa mfumo wa picha, video, an au hata chapisho zima kuhusu bidhaa fulani, nakadhalika.

Uza bidhaa za kidigitali

Ikiwa hutaki kuhangaika kutangazia watu wengine, unaweza kutumia blogu yako kutangaza na kuuza bidhaa za kidigitali mfano vitabu, picha, muziki, video n.k.

Unachotakwa kuzingatia hapa, bidhaa utakazoziuza ziandane na maudhui ya blogu yako na pia mahitaji ya wasomaji wako, hutakiwi kuacha kuandika mambo muhimu kwenye blogu yako na kufanya biashara tu, kumbuka watu wanafungu ablogu yako kujifunza, hivyo biashara iwe ni jambo la ziada ili wasomaji wako wasichukizwe na waendelee kufurahia blogu yako.

Andaa unachama wa kulipia kwenye blogu yako

Unaweza kuwa mbunifu zaidi na ukaandaa uanachama wa wasomaji wako ambao watajisajili na kulipia ili kupata huduma na maudhui ya kipekee zaidi, mfano mwandishi wa habari anaweza kuwalipisha wasomaji wake kupata habari mahususi zenye kuchambuliwa kwa kina na hata kushuhusia mahojiano aliyoandaa na baadhi ya watu mashuhuri.

Jenga jina na hadhi ya weledi wako

Blogu inaweza kuwa ni njia ya wewe binafsi kuonyesha uwezo na ufanisi ulionao katika fani mbalimbali na hivyo ukapata mialiko ya kufanya mafundisho, ama kupata kazi za kimikataba ambayo utakubaliana na wateja wako wakulipe.

 


Nimatumaini yangu nitakua nimejibu baadhi ya maswali kwenye chapisho hili, tadhali usiache kujifunza na kuuliza kama una swali jingine, nami nitakuwa huru kukujibu bila shaka.

Nitanendelea kushirikisha taarifa muhimu na mbinu mbali mbali zinazohusu TEHAMA kwa ujumla, hivyo shirikisha bandiko hili na mengine mengi ili nipate wasomaji wengi zaidi kama wewe na hatimae kuongeza ufahamu wa mambo haya katika jamii yetu.

Tumia program za Windows kwenye Linux!

Linux ni moja kati ya mifumo mashuhuri ya uendeshaji kompyuta, imekua ikitumika tangu miaka ya 1984. Programu hii hupatikana bure kabisa na katika ladha tofauti zinazofahamika kama ditros, kati ya distro maarufu sana duniani ni Ubuntu, Linux Mint, na fedora. Tofauti na Windows au Mac za Apple, kwenye Linux programu zote waweza pata bure pia bila gharama yoyote.

Ingawa ni ya bure, Umaarufu wa Linux pia hutokana na uwezo wake wakutosumbuliwa na virusi (Computer Viruses) kama ilivyo kwenye Microsoft Windows, na uwezekano wa kupata msaada kwenye mtandao kwa urahisi na haraka sana.

Changamoto kubwa kwa wanaoanza ama kuhamia kutoka kwenye Windows na kuanza kutumia Linux, hasa Ubuntu, huwa ni kuzoea muonekano, na zaidi ni kupata programu (Softwares) ambazo alikuwa anazitumia kwenye Windows. Mfano, programu ya Kuchapa (Microsoft Word) na nyinginezo nyingi. Kwenye Linux kuna programu Mbadala ya zile zilizoko kwenye Windows, hata hivyo zinaweza zisifikie kiwango na ubora wa zile za kwenye Windows, lakini kwa kiasi kikubwa zinaweza kukusaidia kufanya unayohitaji kama ambayo ungefanya kwenye windows. Mifano ya programu mbadala zilizoko tayari ndani ya ubuntu ni kama ifuatavyo:-

  • Mozilla Firefox – kuperuzi wavuti, waweza pia kuingiza google chrome
  • Libre Office – mbadala wa Microsoft Office
  • Mozilla Thunderbird – mbadala wa Microsoft Outlook
  • Document Viewer – Mbadala wa Adobe reader
  • Rythimbox Music Player
  • Videos Media Player

 

Nitazungumzia namna mbalimbali ambazo unaweza kuzitumia kwenye linux kufanya kama ambavyo unhgefanya kwenye windows. Njia hizi baadhi zaweza kukusaidia pia hata ikitokea umeenda sehemu na ukakuta kompyuta inatumia mifumo wa linux badala ya windows uliyozoea mfano kwenye Internet Cafe.

1 : Tafuta mbadala wa programu.

Kuna tovuti maarufu sana inaitwa osalt.com, tovuti hii inakuonyesha programu mbadala wa programu nyingi ambazo zinauzwa. Mibadala hii si kwa ajili ya Linux/Ubuntu peke yake, yaweza pia kutumia kwenye Windows, Mfano Ukitaka mbadala wa Microsoft Word, utakuta kuna nyingi ikiwemo, AbiWord, OpenOffice Writer, KWord n.k.

2 : Tumia programu za online

Siku hizi kumeibuka teknolojia ya Cloud Computing ambayo inawezesha mtumiaji wa kumpyuta kutojali kuwa na kifaa fulani tu ili kuona na kufanya kazi zake. Cloud Computing inasaidia pia kushirikiana na wenzako na huna haja ya kubeba kompyuta tena kama unasafiri, ili mradi unakoenda kuwe na kompyuta na mtandao. Hivyo kuna huduma nyingi mtandaoni zinazowezesha wewe kuhifadhi mafaili yako ikiwemo nyaraka, picha, miziki na hata video na ukaweza kuvipata katika vifaa vingi tofauti.

Kwa njia hii unaweza kutumia linux na ukiwa na mtandao basi utachapa barua zako ikiwa online, baadhi ya huduma za bure unazoweza kutumia ni kama:-

  1. Google Drive kuhifadhi mafaili na Google Docs kama mbadala wa Microsoft Office
  2. Drop Box kuhifadhi mafaili yako ya aina zote.
  3. Office Online hii ndio kila kitu kama cha Microsoft Office ila ni online
  4. PIXLR hii ni kwa wale wanotumia photoshop na programu za graphics.

 

Kwa kila ain aya programu, ina mpbadala wake kwenye wovuti, hivyo ni wewe kutafuta tu.

3 : Sanikisha programu kwa kutumia WINE au PlayOnLinux.

Kuna programu inaitwa WINE ikimaanisha “Wine is not Emulator” ambayo inakuwezesha kusanikisha(Install) programu za Windows moja kwa moja kama vile iko kwenye Windows. Programu hii unaweza kuitafuta ndani ya Ubuntu kwa jina la Wine au PlayOnLinux. Ukishakuwa nayo unaweza kusanikisha baadhi ya programu muhimu kama Microsoft Office, Adobe Photoshop, na nyininezo nyingi.

4 : Sanikisha Windows kwenye Virtual Machine

Kwa kuwa Linux/Ubuntu inahakikisha usalama zaidi dhidi ya virusi vya kompyuta, na iko haraka kuliko Windows, unaweza pia ukaingiza Windows ndani ya Ubuntu kwa kutumia programu maalumu inayoitwa Virtual Box. Virtual Box inaweza kutengeza mfano wa kompyuta nyingine (Virtual Machine) ndani ya kompyuta yako uliyonayo, halafu ukaingiza windows na ukatumia programu zako unazotaka endapo njia nilizoordhesha hapo juu hazikufaa.

ZINGATIA: Hatua hii ya kutumia Virtual Box waweza pia kuifanya ndani ya Windows na ukasanikisha ubuntu ili kuijaribu na kujifunza kabla haujaamua kuitumia rasmi.

Bila shaka umeweza kupata angalau uelewa wa namya kutumia baadhi ya programu uzipendazo kwenye Windows ndani ya Linux. Kwa maoni, maswali na ama ushauri usisite kuniandikia kwenye fomu ya maoni hapo chini, ama kutuma ujumbe wako kwenda info@webnerdtz.com

Mfumo wa uendeshaji kompyuta

Mfumo wa uendeshaji kompyuta (Computer Operating System) ama waweza kuita mfumo endeshi ya kompyuta ndio programu muhimu inayowezesha kompyuta kufanya kazi. Mfumo huu ndio unasimamia vifaa vyote kwenye kompyuta na kuwezesha programu zingine kutumia vifaa hivyo kutimiza kazi inayopaswa kufanya. Inasimamia kumbukumbu, michakato na kila kitu cha kukurahisishia wewe mtumiaji kuwasiliana na kompyuta pasi na kufahamu lugha yake. Bila mfumo huu, kompyuta haina maana, na isingeweza kuonekana kifaa matata kama kinavyoheshimika, ni mfumo huu wa endeshaji haswa ndio kila kitu.

Kazi kuu ya mfumo endeshi wa kompyuta

Mfumo huu unawajibu wa kusimamia vifaa vyote vilivyopo kwenye kompyuta, kuhakikisha kila programu zilizofunguliwa na zitakazofunguliwa zinapata nafasi ya kutumia vifaa kwa uwiano ulio sawa. Programu hii pia ina hakikisha wewe mtumiaji unaweza kuwasiliana na kompyuta kwa kukupatia njia ya kuitumia (interface), mfano wengi tumeozoea kuona mshale wa kapuku(mouse) na ikoni vya kubonyeza ili kufungua au kufunga dirisha(window) la programu kwenye kompyuta, Ama wengine kompyuta zao huzipa sehemu ya kuandika amri(commands) za kuifanya kompyuta ifanye kazi fulani.

Aina za mifumo endeshi ya kompyuta

Kompyuta nyingi za watumiaji wa kawaida huuzwa zikiwa na mfumo endeshi tayari, hata hivyo unaweza kubadilisha au kuboresha(upgrade) mfumo endeshi uliomo. Kati ya mifumo endeshi maarufu kwenye kompyuta binafsi ni Microsoft Windows, Linux, na Apple Mac OS X. Mifumo hii ya kisasa ni yenye kutumia muonekano unaofahamika kama Graphical User Interface (GUI) ikimanisha muonekano wenye grafiki ambao unakuwezesha kutumia kipanya kubofya ikoni(icons), menyu, na matini(text).

Kila mfumo endeshi unamuonekano na ladha yake, ingawa ina fanania na zote zimefanywa kuwa rahisi kutumia, lakini ukibadili kutoka mfumo endeshi mfano wa Windows kwenda wa Linux kama ubuntu utaweza kupata tabu kidogo mpaka uzoee munekano huo kwa muda kidogo.  Kabla y amuonekano wa grafiki, kompyuta zilikuwa zikitumia muonekano wa giza tu na kupwatia mtumiaji mstari wa amri (Command Line Interface), hivyo mtumiaji alipaswa kuandika kila kitu kwa kutumia kibodi tu, hakuna kubofya kwa puku (Mouse).

Mirosoft Windows

Mfumo huu umetengezwa na kampuni ya Microsoft kati kati ya mwaka 1980, na tangu kuanza kwake, Windows imekua na mateoleo mbali mbali yenye kuakizi kukua kwa tekinolojia na ubora wake.

Ni Programu endeshi maarufu sana duniani, na toleo la hivi karibuni ni Windows 10, ya nyuma yake ni Windows 8, Windows 7, na Windows Vista. Pamoja na matoleo hayo pia utataka kujua kama Windows hiyo ni kwa matumizi ya Nyumani (Home Edition), Mabigwa (Professional Edition), au Mwisho (Ultimate Edition), ni muhimu ukafuatilia haya ili ujiridhishe kulingana na matumizi yako.

understandos_windows

Muonekano wa Mikrosoft Windows 7

Mac OS X

Mfumo endeshi huu umetengezwa na kampuni inayotwa Apple Inc., moja ya makampuni maarufu kutokana na bidhaa zake kuwa za ghali, na za kipekee, zina mionekano mzuri sana ukilinganisha na Programu Endeshi zingine. Kulingana na takwimu za matumizi kutoka statcounter.com 2016, OS X ina 9% ukilinganisha na Windows ambayo ina zaidi ya 50%. (angalia futiko la takwimu mwisho wa makala hii)

understandos_os_x

Muonekano wa Mac OS X

 

Linux

Linux ni mfumo endeshi ambao hufanywa kama programu za chanzo huria (open source), watu na makampuni mbali mbali duniani hutenegeneza ladha tofauti juu ya programu endeshi ya linux, hivyo hakuna kampuni maalumu kama ilivyo Microsoft kwa Windows au Apple kwa Mac OS X. DistroWatch.com. inaorodhesha mateleo takiribani 100 ya Linux, ambapo matoleo maarufu zaidi ni Ubuntu, Mint, na Fedora.

FHv2w

Muonekano wa Ubuntu

Mifumo endeshi ya vifaa vya mkononi

Vifaa vya mkononi kama simu hasa za kisasa, kompyuta kibao (Tablets) na kadhalika, havitumii programu endeshi kama hizo tulizoziona hpo juu, zenyewe hutumia programu endeshi maalumu kwa ajili ya kifaa hicho, na hazina uwezo wa kufanya kila kitu kama hizi zingine. Mafano wa programu endeshi maarufu kwa simu ni Google Android, Apple iOS, na Windows Mobile.

Hitimisho

Leo umepata kufahamu mifumo endeshi maarufu ya kompyuta, na jinsi gani mifumo hiyo iko maarufu kwa watumiaji duniani. Kwenye makala zinginezo utapata kujifunza namna ya kufanya mambo mbali mbali ikiwa kompyuta yako una mfumo mmoja wapo ya hio. Nakucha na takwimu za matumizi kwa ufuatliaji na kujifunza zaidi hapa.

 

Source: StatCounter Global Stats – OS Market Share

Kompyuta ni nini?

Umeanza kutumia kompyuta?, je una maswali unaposikia watu wanasema maneno na misamiati ya kompyuta na ukashindwa kuelewa?, bas makala hii itajadili mada yenye kutambulisha kwako mambo muhimu yanayohusu kompyuta. Usiwe na hofu, kwa sababu tulipofikia kwa sasa hatuwezi kukwepa kutumia kompyuta, hivyo ukiwa na uelewa kidogo tu utakaojifunza hapa, utafahamu kompyuta ni nini na utabaini aina mbali mbali za kompyuta zilizopo. haya tuanze kujifunza. Kompyuta ni nini?

Kompyuta ni kifaa cha ki elektroniki ambacho hufanya kazi kwa kuendesha taarifa, au data. Kifaa hichi kina uwezo wa kuhifadhi, kuchambua, na kuchakata data/taarifa. Bila shaka unafahamu kuwa waweza tumia kompyuta kuchapa nyaraka mbalimbali, kutuma barua pepe, kucheza michezo, na kuvinjari mtandaoni. Waweza pia kutumia kompyuta kuhariri picha, video na mambo mengine mengi. Tafadhali angalia picha hii hapa chini kuona watu mbali mbali wakitumia kompyuta (Picha hii nimeitoa mtandaoni kwanuani hii).

computer_grid

Vifaa na Programu za Kompyuta.

Kabla hatujajifunza aina za kompyuta, tujifunze vitu/mambo muhimu yanayokamilisha kompyuta. Kumpyuta ina sehemu kuu mbili, Vifaa ( Hardware ) na Programu (Software).

Vifaa(Hardware) vinashikika na ndio vinaunda mifumo ya ki elekroniki ambayo inaonekana kifizikia mfano, kipanya(mouse), kiambaa (keyboard), Kioo cha kuangalizia (Monitor/screen) na vyote vilivyomo ndani ya kasha la kompyuta.

Programu(Software) hazishikiki, ni mkinyaiko wa maelekezo ya kuviongoza vifaa vifanye kazi na kusababish amatokeo ambyo mtumiaji anataka yatokee kwenye kila jambo. Mfano wa programu ni kivinjari cha wavuti  (web browser) au programu ya kuandika nyaraka ya Microsoft Word, na zingine nyingi ambazo tutajifunza huko mbele. Kimsingi hizi programuu ndizo zinazofanya watu wafurahie na wanufaike kutumia kompyuta lakini zitafanya yote juu ya vifaa vyenye uwezo wa kupokea maelekezo hayo.

Chochote unachofanya kwenye kompyuta hutegema vifaa na programu. Mfano hivi sasa yawezekana unasoma makala hii kwa kutumia kivinjari (web browser) ikiwa ndani ya kompyuta ya mezani, na unatumia kipanya(mouse) kubofya viungo vilivyomo kwenye kurasa ili kufungua kurasa zingine kwenye tovuti hui au nyinginezo. Na baada ya kujifunza aina za kumpyuta utajiuliza kwenye aina tofauti za kompyuta hizo ni vifaa gani vinaweza kutumika kama kipanya.

Aina za kompyuta

Wengi wanaposikia kompyuta huelekeza mawazo yao kwenye kompyuta za mezani (Desktop Computers) au kompyuta za mpakato (Laptop Computers), lakini ukweli ni kwamba kuna aina nyingi za kompyuta zaidi ya hizo mbili nilizokwisha zitaja hapa. Na kwa maendeleo ya tekinolojia yalipofikia hivi sasa, ni muhimu ukafahamu kuwa kompyuta zimetuzunguka kila mahali, ziko mezani, mikononi, barabarani, hospitali, na kila mahali.

Kimsingi kompyuta zimegawanyika katika makundi makuu mawili, kuna kompyuta za madhumuni ya jumla (General purpose computers) hizi ndio wengi wanazitambua na kuzibainisha moja kwa moja kama kompyuta, lakini pia ziko kompyuta za kusudi maalumu (Special purpose computers) mfano, kikokotozi (calculator) ni kompyuta kwa ajili ya kukokotoa tu. Vifaa vingi vya eletroniki mfano luninga (TV), Saa za digitali (digital watches), kisimbuzi (decoders), simu za mkononi za kawaida (feature phones) zina kompyuta maalumu kwa kazi yake, na zina uwezo wa kuhifadhi, kuchakata, na kuendesha data kulingana na mipaka yake.

Tujifunze sasa baadhi ya kompyuta ambazo wengi huzibainisha moja kwa moja, mada yakuelekeza aina zote za kumpyuta na zinavyofanya kazi iko inje ya makala hii, badala yake tutaangazia zaidi kompyuta zinazotumiwa na watu binafsi zaidi (personal computers), kama zifuatavyo.

Kompyuta ya mezani (Desktop Computer)

Hizi utazikuta sana maofisini, majumbani, mashuleni nakadhalika, zinakaa juu ya meza, zaweza kuwa ndogo, saizi ya kati, au kubwa sana kimuonekano lakini umbile sio lazima lishabihiane na uwezo, tutakuja kujifunza sifa zinazoipa uwezo kompyuta kwenye makala nyingine. Mara nyingi iko pembeni ya Kioo cha kungalizia (monitor) , pia imeunganishwa na kipanya (mouse), na kiambaa (keyboard).desktop-computer1

Konpyuta ya mezani ni rahisi kuiboresha kwa kuongezea vitu, na pia bei yake ni rahisi kwa sababu vifaa vyake hutengezwa kwa maumbile makubwa kiasi ambvyo kitekinolojia sio ghali kuvitengeneza ukilinganisha na vifaa vya kompyuta ndogo kiumbo. Uliknganisha kumpyuta ya mezani na ya mpakato zenye uwezo sawa, utakuta ya mezani ni ya gharama nafuu sana kwa bei.

Kompyuta ya kupakata (Laptop computer)

Hii ni aina ya pili maarufu ya kompyuta binafsi, ni ndogo na zinabebekam hivyo waweza kuzitumia karibu kila mahali uendapo kwa sababu zinatumia betri ya kuchaji. Mara zinatuza chaji kwa muda zaidi ya masaa mawili, hivyo wengi wanafurahia kuzitumia kwa uhuru wa kuweza kutembea nazo. Lenovo-Notebook-İndirimi1

Kutokana na udogo wake sio rahisi sana kuziongezea au kubadilisha vifaa vyake vya ndani kama ambvyo ungefanya kwenye kompyuta za mezani, inagawa inawezekana, alini huwa zimetengezwa na sifa zenye kuifaa ikiwa hivyo, labda itokee kifaa kimeharibika.

Kipanya na kiambaa ni sehemu ya kompyuta hii, ila pia waweza kuunga vifaa vya pembeni endapo utahitaji.

 

Kompyuta Kibao (Tablet computer)

Kompyuta kibao ni kompyuta ndogo zaidi ya kompyuta mpakato, yenyewe ni ya kushika mhononi tu, na rahisi zaidi kutembea nayo popote, na huwa zikikaa na chaji kuliko za kupakata. Badala yakutumia kipanya na kiambaa, yenyewe unagusa na vidole vyako kwenye kioo ili kuandika au kuperuzi, pia zingine huwa na kalamu maalumu (Stylus) unayoweza kuchora au kuandika juu ya kioo chake. iPad ni mfano wa kompyuta maaarufu ya namna hii.Apple-tablet-computer-con-001

Kompyuta hizi, hafinayi kila kitu ambacho ya mezani au ya kupakata yaweza fanya, lakini waweza kuitumia kama unataka kujisomea, kucheza michezo, kuwasiliana na watu kwenye mitandao ya kijamii, kusoma barua pepe, na kujiburudisha kwa kusikiliza miziki na kuangalia video. Kutokana na muundo na malengo ya matumizi yake, hazina uwezo mkubwa wa kuhifadhi na kuchakata data, na utaifurahia zaidi kama utakuwa na mtandao wa wavuti(internet), kwa mtu mwenye kuihitaji burudani na kupata taarifa kwa urahisi popote alipo, kompyuta hizi huwafaa sana, lakini bado utahitaji kuwa na ya mezani au ya kupakata ili uweze kufanya kazi zingine za kompyuta kama kuchapa nyaraka n.k.

Seva kompyuta (Server)

Seva ni kompyuta ambayo inahudumia kompyuta zingine zilizo kwenye mtandao, mtandao unaweza kuwa wa ndani ya ofisi (local area network), au mtandao wa wavuti (internet). Makampuni mengi yanatumia seva kuifadhi mafaili na kutoa huduma zigine kwa wafanyakazi na pia kitoa taarifa kwa wateja mbalimbali. Seva yaweza kuonekana kama kama kompyuta ya kawaida au yenye umbile kubwa zaidi, na kwenye makampuni makubwa seva hutengawa kwenye vyumba maalumu na hutunzwa kwa mumakini mkubwa kwa sababu zintegemewa na mamilioni ya wahiyajio huduma.computer-servers

Seva ndio mchezaji mkuu wa mtandao, ndio wanaofanya watu kuwa na tovuti duniani, na ndio vichochezi vya tekinolojia ya wingu la makompyuta (cloud computing). Unapoangalia muziki kwenye tovuti ya www.youtube.com video zote hizo zimehifadhiwa kwenye seva, na seva inakuhudumia video unayotaka kuiona kwenye kompyuta yako, ba inafanya hivyo kwa ziadi ya kompyuta milioni kwa wakati mmoja, hivyo seva zina uwezo mkubwa sana wa kuhifadhi na kuchakata data, na ni gharama kuziunda, na kuzitunza pia.

 

 

Aina nyigine za kompyuta

Kama nilivyogusia awali, leo hii kuna aina lukuki za kompyuta ambazo kwa kiasi kikubwa ni za matumizi maalumu. Ili kuongezea elimu yetu hii, nitaorodhesha baadhi ya kompyuta hizo:-

  1. Simu za mikononi – wengi wanatumia simu za mikononi za kisasa (Smartphones) kufanya mambo mengi amabyo ungeweza kufanya kwenye kompyuta ya mezani kama kucheza michezo (games), kusom abarua pepe, na kuangalia mztandao pia kuwasiliana na marafiki kwenye mitandao ya kijamii
  2. Kumpyuta za michezo (Game consoles) – mfano playstation, nintendo n.k, hizi ni kompyuta maalumu kwa michezo ya kwenye luninga, mfano mpira, magari n.k.
  3. Luninga (TV) – hizi za kisasa zinauwezo wa kuunganisha kwenye mtandao wa wavuti na kufungua taarifa mbali mbali

Hitimisho

Tumejifunza kompyuta ni nini?, na watu hutumia kompyuta kufanya mambo gani, pia tumeona baadhi ya aina mbali mabli za kompyuta na kufahamu matumizi yake na mipaka yake kwa ujumla. Somo hili halitaishia hapa kwani bado kuna mengi ya kujifunza kuhusu kompyuta hizi, kwenye makala nyingine tutajifunza kuhusu uwezo wa kumpyuta na unaweza vipi kufahamu, pia sifa za programu endeshi za kompyuta hizo.

Tafadhali anedela kufungua tovuti hii ili uweze kujifunza zaidi kuhusu mambo ya TEHAMA.

How to add currency format in MS Excel.

Hi there, Today i will show the simplest and ultimate way of adding none available local currency format in Microsoft Excel. This actually a Windows tip in general, for some countries like Tanzania we don’t have a currency symbol like $ which are special characters, so we have for example TShs 800.00.

You may ask your self how can you have column in Excel which display numbers formatted in local currency like shown below?,

When you finish the colum will look like this.

When you finish the column will look like this.

how to achieve that is what i am going to tip you, and at the end there is a video for you to watch the steps i followed when setting up currency format for Tanzanian Shillings, but it can be done for any other formats as well, its just a matter of preference.

Step 1:

In your excel sheet highlight the column that you want to format and put it to the currency format as shown below:

excel_selection

Step 2:

Open Windows Control Panel and click on the Regions option, on the dialog that appears click on Additional Settings button:

region_1

Step 3:

On the Additional Settings Dialog that appears click on the Currency Tab and Edit the Currency Symbol as shown below:

currency

After that Click Apply and then Ok buttons on both dialogs. Now you will see your sheets column in displayed with the new currency format. Watch this video for more visual demo.

I hope this tip will help someone, keep following this blog for tips like this.,

VIDEO: Tumia Windows kwa Kiswahili

Habari, Je!, wewe ni mpenzi wa lugha ya kiswahili?, na ungependa kutumia kompyuta yako au kifaa cha cha windows kikiwa na lugha hiyo?. Mikrosoft windows ana kifurushi cha lugha yetu pendwa na kinaweza kutumika kwenye kompyuta yako.

Kwenye makala hii nitakuonyesha namna unaweza kufanya kompyuta yako yenye Windows 8 ambayo pia inafanana na baadhi ya vifaa vya Windows Mobile iwe kwa lugha ya kiswahili, na hata lugha nyingine pia kama utapenda, namna ya kufanya hivyo hakutofautiani sana.

Utahitaji kuwa mtandaoni na kifaa chako, ili uweze kupakua kabrasha la lugha, ba baada ya kuingiza lugha kama utakavyoona, itabidi utoke (sign out/logout) na uingie tena(sign in/login) ili kuona mabadiliko ya lugha kwenye kifaa chako.

Angalia video hii hapa chini kujifunza.

Jinsi ya kusanikisha Movie Maker kwenye Windows 8

Habari wadau, ni muda sasa umekwenda lakini si mbaya leo tukijifunza kitu pia. Umewahi kujiuliza Video zinafanyiwa vipi editing?. Kama ndio bila shaka umeshafahamu kuwa Editing inafanyika zaidi kwenye Computer, na kuna programs au software ambazo nyingi ni ghali kuzinunua ambazo zitakuwezesha kufanya jambo hilo.

Kabla hatujazifahamu programu zinazotumika kwa shughuli hiyo, kwanza tujifahamishe kuhusu sifa zake za msingi. Programu ya Editing inategemewa kukuwezesha mtumiaji kufanya mambo yafuatayo:

  • Kuweza kufanyia kazi aina tofauti za mafaili utakayokuwa nayo, na kuweza kuyabadili mafaili hayo kwenda kwenye mfumo mwingine; aina za mafaili ni kama avi,mp4,mpg,jpg png,mp3 n.k
  • Kuunganisha vipande vya video, kukata sehemeu za video ambazo hutaki ziwepo na kuziondoa,
  • Kufanya angalau baadhi ya marekebisho kwenye sauti ya video ikiwa ni pamoja na kuongeza sauti ya ziada kama voice-over, athari za sauti na muziki wa nyuma kwenye video hiyo
  • Kufanya angalau marekebisho ya muonekano wa video husika, kama vile mwanga n.k, hapa tunazunguzia filters na effects mbalimbali ambazo zitapendezesha video yako machoni kwa watazamaji.
  • Kuwa na uwezo wa kuongeza mabadiliko kati ya sehemu za video zilizo katika mtiririko wa hadithi mfano picha kufifia, kupunguzwa, unafifia na nyeusi, unafifia na nyeupe n.k.
  • Kuwa na uwezo wa kuongeza maneno na vijimaneno kwa udhibiti mzuri na makala aina mbalimbali kwa ubunifu.

Hizi ni sifa za msingi kuwa nazo katika programu ya kurekeishia video zako. Hivyo kama una kamera nzuri inayoweza kurekodi video safi na una kompyuta nyumbani bila shaka utatamani kutumia programu hizi ili kupunguza gharama, maana waweza rekebisha video zako na kuzichoma kwenye CD na ukahifadhi kumbukumbu zako kisasa zaidi, au sio?.

Kwa ujumla ziko programu nyingi maarufu, na kama nilivyokwisha bainisha awali ni kuwa nyingi kati ya hizo zinauzwa na zina mambo mengi ya ziada ambayo si ya lazima sana kuwa nayo kwa video zako za nyumbani, hivyo Microsoft Windows huwa inawapatia watumiaji wake programu ambayo ni bure na inakuwezesha kufanya yote ya msingi.

Programu hii inaitwa Windows Movie Maker na kwa bahati mbaya inaweza isiwepo kwenye baadhi ya kompyuta zenye programu endeshi ya windows. Kama haipo kwenye kompyuta yako pia nenda hapa kuipakua kulingana na toleo la Windows yako. Utaipakua na kisha kuisanikisha kwa kufuata maelekezo yake.

Ukiifungua programu hiyo itaonekana hivi:

mm

Movie Maker Ikifunguka

Ni matumaini yangu utaweza kujifunza zaidi jinsi ya kuitumia programu hiyo kwa iko rahisi na vitu vyake viko wazi sana kuielewa, na pengine waweza kuja kuwa editor mzuri zaidi hata ukapata hamu ya kutumi programu kubwa za aina hii.

Endelea kufurahia kompyuta yako.

Usiogope kufungua tovuti sababu ya utofauti wa Lugha!

Ndio, nafahamu kuwa tovuti nyingi zina lugha za kigeni, tena tovuti hizi mara nyingi ndio zenye tija hasa!, lakini watumiaji wa kitanzania walio wengi wanafahamu kingeereza pia, vipi sasa wakikuta tovuti ina lugha ya kifaransa ama kireno, au kichina kabisa?, Kwa harak haraka mtu huyu atafunga tu huo ukurasa na kuperuzi kurasa zingine!

Usiogope, unaifahamu GOOGLE sio?, basi ni rahisi sana, google wana kifaa murua sana unachoweza kukitumia ili kuweza kutafsiri, sio tu tovuti nzima bali hata neno mojamoja. Ni rahisi sana wewe kwenye kivinjari (Browser) chako andika anuani hii http://translate.google.com waweza kubonyeza hapa pia. Ukurasa kama huu hapo chini utafunguka, chakufanya andika neno ambalo unataka litafsiriwe upande wa kushoto halafu chagua lugha ya tafsiri upande wa kulia na utaona tafsiri yake.

Ikiwa kuna tovuti ungependa itafsiriwe waweza kuandika anuani ya tovuti hiyo mfano http://www.france.fr/ upande wa kulia itatokea neno hilohilo kama kiungo, basi bonyeza(click) kiungo hicho na utaona ukurasa huo unafunguka kwenye lugha ya tafsiri.

Waweza pia kukopi na kupesti ukipenda ili kuona tafsiri.

DONDOO: Unaweza andika hadithi yako ya kiswahili ambayo wataka iwe kwa kingereza kwa kutumia kifaa hichi kwa urahisi sana!, nimekuwa nikijaribu kufanya hivyo mara nyingi sana kipindi nipo shuleni!.

Bila shaka kifaa hichi cha mtandaoni kitakuwia manufaa sana. Waweza pia kutazama video hii kujifunza zaidi:

Jinsi ya kuanzisha Blogu – hatua kwa hatua!

Mimi najua, kuanzisha blogu inaweza kuwa na utata. Miaka michache iliyopita, wakati mimi naunda blogu yangu ya kwanza, nilikuwa najua machache kuhusu matumizi ama umuhimu wake. Kwa kuwa nilikuwa ni msomi wa kompyuta hivyo nilishaona mara kwa mara blogu zikitoa maelekezo juu mambo mbalimbali yahusuyo na hata yasiyohusu kompyuta.

Kwa sasa, nimekuwa nikishuhudia blogu nyingi zikianzishwa, zingine zikiwa na maudhui mazuri na yenye tija kubwa kwa jamii yetu, na nyingine zikiwa hazina cha maana kabisa. Wingi wa blogu na utembelewaji wake unaashiria kiu ya wengi kumiliki blogu na kupashana taarifa mbalimbali.

Ninachoweza kusema ni kwamba kujenga blogu ni rahisi sana na hauhitaji ujuzi wowote kutengeneza tovuti wala kuchapa kodi!. Kwa kweli, mchakato mzima ni kiasi fulani moja kwa moja. Hivyo kama wewe uwe na  umri wa miaka 20 au miaka 70, si jambo – bado unaweza kufanya hivyo ndani ya dakika kumi tu!. Unaweza kufanya hivyo pia, tu kwa kufuata hatua zifuatazo.

 

TAFADHALI:. Kama utakwama au utahitaji msaada kuanzisha blog yako, usisite kuwasiliana nami, nitakuwa tayari kukusaidia bila shida na kwa gharama nafuu.

 

Tuanze?

1) AMUA NINI BLOG YAKO ITAHUSU

Jambo la kwanza unahitaji kufanya ni kuchagua mada ya blogu. Je, kuna jambo ungependa watu walifahamu?, Kama ndio, anzisha blogu kuhusu hilo. Ni bora kama wewe umebobea katika nyanja fulani na hata umekuwa kwenye sekta fulani kwa muda mrefu, na kwa sababu hiyo wewe ni mtaalam, unaweza kujaribu blogu itakayoelimisha watu wengine wenye kupenda kuwa kama wewe.

Hata hivyo, kama una wazo lolote ambalo mada yake inaelekeza fursa ya kupata wateja mfano mpishi anaweza kuandika habari za mapishi huku akilenga kupata tenda za mapishi kupitia wasomaji wa blogu yake. Fikiria jambio ulipendalo sana,  au kuwa balozi kuhusu shughuli za kila siku.

 

2) AMUA NI NAMNA GANI UTAHODHI BLOGU YAKO, UTALIPIA, AU YA BURE?

Awali ya yote, blogu nyingi kwenye mtandao ni kwa kutumia WordPress. Kwa kweli, WordPress imepakuliwa zaidi ya mara milioni 72 na hutumiwa na mabloga wengi maarufu na tovuti mbalimbali ikiwemo na hii unayoisoma sasa.

Ni kwa nini nadhani kutumia WordPress ni njia bora ya kuanza blogu yako:

  • Unaweza kuchagua mandhari (Themes) na mipangilio (Layouts) kutoka kwa watu wengi tofauti na bure.
  • Unaweza kuandika makala kwa urahisi na kuongeza picha / video
  • Una uwezo wa kuandaa kategoria na kujenga orodha makabrasha (Archives)
  • Watu wanaweza kutoa maoni na kushiriki blog yako
  • nk …

  Bure si BURE …

Ndiyo, unaweza kuunda blogu ya bure kwenye blogger.com au tumblr.com , lakini wao si kweli bure. Na napenda kukuambia kwa nini …

Wao wana upungufu wa mandhari nzuri – Kwa maneno mengine, blog yako itakuwa ikionekana tupu na kawaida. Kama unataka mandhari ya ziada au vipachiko (Plugins) vya kuboresha blogu yako, unatakiwa kulipia vitu hivyo.

 Huna udhibiti wa blog yako – blogu yako itakuwa ni mwenyeji kwenye tovuti nyingine, hivyo wewe si “mmiliki” wa mali hii. Kama Wasimamizi wakiamua kwamba blogu yako haiendani na sera zao (ambayo inaweza kutokea mara nyingi kabisa), wanaweza kweli kufuta blogu yako bila maonyo yoyote. Kwa kifupi, kila kazi yako uliyofanya kwa bidii bidii na muda alitumia juu ya blogu itakuwa vimepotea ndani ya sekunde.

Gharama ya kuanzisha BLOGU yenye domain yako mwenyewe NI NINI?

Si sana. Unahitaji domain mfano (jinalako.com) kwa  gharama takriban TShs 30000 kwa mwaka na hosting (huduma unajumuisha blog yako na mtandao) ni karibu TShs 75000 – 150000 kwa mwaka. Jambo zuri kuhusu domain binafsi kwa blogu yako ni kwamba pia utaweza kuwa na mawasiliano ya barua pepe yenye mfano wa jina@lako.com.

3) KUCHAGUA DOMAIN & hosting, na KUANDAA WordPress blog domain yako mwenyewe

Kama aliamua kwenda na blogu yenye  domain yako mwenyewe, utahitaji kuchaguajina la domain yako ambalo litaendana na blogu na pia liwe rahisi kukumbukwa. Kupata jina zuri la domain inaweza kuchukua muda., Lakini ni thamani yake.  Lakini kwa nini?

Watu hawawezi kukumbuka domain muda mrefu na wakati wanataka kurudi kwenye blogu yako kuna uwezekano wa kusahau jina hilo. Ni bora zaidi kuchagua kitu cha kukumbukwa, kama vile www.fashionologie.com, www.vivalafashion.com au kitu sawa. Kama mbadala, unaweza tu kutumia jina lako, kwa mfano:. www.johnkipepeo.com

Kwa kifupi, jina la domain yako lazima:

  • Livutie
  • Rahisi kukumbuka
  • Lakipekee

WAPI NAWEZA KUPATA JINA LA DOMAIN NA HOSTING?

Mimi kawaida hupendekeza watu kupata domain na hosting kutoka sehemu moja, kwa njia ambayo itasaidia kuokoa baadhi ya fedha na wakati. Katika miaka michache iliyopita wakati mimi naanza kujenga na kusimamia blogu mbalimbali, nimegundua kwamba kuna makampuni machache sana yakuaminika.

Kuwa muwazi zaidi, nimekuwa nikitumia makampuni kadhaa katika siku za nyuma. Kutaja baadhi yao: Bluehost, Hostgator, Dreamhost nk LAKINI … Mimi sikuwahi kuridhika na huduma yao. Hivyo kwa urahisi napenda kukuelekeza WEBNERD SOLUTIONS ili upate huduma hizo kwa gharama nafuu.

 

HITIMSHO

Ni matumaini yangu nimejaribu kukufungulia baadhi ya mambo muhimu yanaweza kukusaidia kama unafikiria kuanzisha blogu yako. Tafadhali kama una swali au maoni tumia fomu iliyo hapo chini kuacha maoni yako au swali lako.

Jinsi ya kuitumia google kupata unachokihitaji kirahisi zaidi!

Habari,  tovuti hii www.google.com ni moja kati ya zana zangu muhimu sana tangu nianze kutumia wavuti(internet). Achilia mbali kutafuta mambo mbalimbali, pia napata hiduma nyingi sana ambazo nitakuwa nawaeleza kadri siku zinavyokwenda, kwa leo ningependa kuhusisha njia ninazozitumia mara kwa mara kupata ninachokitaka kirahisi zaidi.

1. kitufe cha leo ni siku yangu (i’m feeling luck)

Kitufe hiki hutumika endapo unataka kupata kitu fulani na kifunguliwe kabisa, mfano: fungua google, kisha andika “Tanzania” kisha bofya(click)  kitufe(button) hicho, hapo utapelekwa moja kwa moja kwenye ukurasa ambao google huhisi ndio hasa unaoutaka, mara nyingi ni ule ukurasa wa kwanza kupatakana kipindi inatafuta. Ni njia ndogo na unaweza usione umuhimu wake ila kama neno ulilotumia kutafuta uko na uhakika nalo basi utapata unachokitaka bila haja ya kuanza kujiuliza kama ambavyo utabofya kile kitufe kingine.

2. Tafuta kwa picha (Image Search)

Ilishawahi kusemwa kwamba picha hubeba maelezo mengi kuliko maandishi, ikiwa unataka kutafuta kitu na umefanya hivyo kwa njia ya kawaida na unapata shida kukibainisha, basi tumia huduma ya kutafuta kwa picha, maana utakacho kiona pengine ndicho na ukiibofya tu basi inakupeleka ulikokutaka bila shida. Mimi binafsi nilipotelewa na mtu(rafiki) kwa kipindi kirefu na nilitumia huduma hii nikampata mara moja, kwa picha zake alizowahi kuzirushia facebook. inasaidia sana ukitafuta kitu kwa picha!

Mbali na kutumia picha, pia unaweza kutafuta kwa kutumia Ramani(Maps), Habari(News), Maswali na Majibu (Q&A) na mengine mengi.

3. Tumia viunganisho kama & || “”

mfano unataka kutafuta dr. slaa, ukiandika hivyo google itakuletea kurasa zenye neo dr na zenye neno slaa ndani yake, hii inaweza kuwa haitoshi kwako na ikakujazia kurasa nyingi na pengize hakuna unyoitaka hata, basi andika hivi “dr. slaa”, hapo itakuletea kurasa zenye neno hilo kama lilivyo na pengine utapata ulichokitafuta vyema kabisa.

Ikitokea unataka  kupata kurasa zinazo muhusu dr slaa, chadema, n.k, basi fanya hivi: “dr. slaa” & “chadema” hapo utapata kurasa zenye neno dr slaa  na chadema, la! pengine unataka dr slaa au chadema basi andika hivi: “dr. slaa” || “Chadema” hapo utapata kurasa zenye neno dr.slaa au zenye chadema.  Viunganisho hivi vinafurahisha sana, mara nyingine unajua ukitafuta dr. slaa, basi kurasa zitakazokuja kwa vyovyote vile zitakuwa na chadema, lakini hutaki hivyo pengine umeshaziona zote, na hamna utakacho, ila bado unataka kupata zenye dr. slaa bila chadema au zenye chadema bila dr. slaa, basi andika hivi: “dr. slaa” XOR “chadema”hapo google itakuletea zenye kimoja kati ya hivyo lakini si zenye vyote tofauti na hapo, italeta kurasa chache sana (raha!).

NB: & = AND, || = OR, nimetumia dr slaa na chadema kama mfano, ni vigumu sana kupata dr slaa bila chadema katika ulimwengu  huu tuliopo sasa!

4. ufafanuzi ( definitions)

Kipindi niko chuoni, google ilinisaidia kufahamu vitu vingi sana kirahisi. Tuseme nataka kujua chakula(food) ni nini?, basi huwa naandika hivi:-define:food, hapo google itaniletea fafanuzi(definitions) kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kwa kifupi ambapo nikipata moja inayonipendeza naweza kufungua tovuti yake nikajifunza zaidi, maisha yalikuwa rahisi sana kwangu, si unajua walimu wengine huwa wana-complicate hizi definitions, pale utapata ambazo ni rahisi na za kueleweka mno.

hii huwa bora zaidi kama unatafuta kwa kiingereza na kuna maneno mengi unaweza kupachikia kabla ya mkato mkuu(full colon) kama about, where, index of, n.k.. kama define linavyotumika.

5. Tafuta kwa aina ya faili kama (pdf, chm, mp3, wav)

kuna wengine huwa watafuta kitu bila kubainisha ni aina gani ya kitu anatafuta, mtafuta vitabu anaweza akapata vitabu kirahisi kama atandika jina la kitabu kisha mabano ndani akaweka extension ya kitabu anachikitafuta mfano: food and drinks book ( pdf || chm), hapo utaletewa kurasa zenye vitabu au viungo vya kitabu vya kusomeka kwa Adobe reader (pdf) au vile vya windows help viwer (chm).

Bila shaka nitakuwa nimehusisha mojawapo ya njia zinazonifurahisha na kunisaidia sana ninapotumia wavuti kwa kujifunza, kujitaarifu,kujiburudisha pia. Zijaribu njia hizi kama hukuwahi kuzifahamu hapo awali, na endelea kupitia tovuti hii kwa kujifunza mambo mengine mengi zaidi.

© 2024, WEBNERD SOLUTIONS