Unawezaje kupata pesa au faida kwa kumiliki blogu?

Unataka kutenegeneza pesa kirahisi sio?, bila shaka, kila mtu anataka kutengeneza pesa halali imsaidie kusukuma maisha yake ya kila siku. Pengine umewahi sikia kuwa ukimiliki blogu ama tovuti unaweza kutengeneza pesa kirahisi?, ndio yawezekana kutengeneza pesa kirahisi kwa kutumia blogu, ila usiwe na shauku sana maana si rahisi tu. Wasomaji wangu wengi wamenitumia ujumbe na wengine kunipigia simu kuuliza nawezaje kupata pesa nikiwa na blogu yangu? Leo nitakushirikisha baadhi tu ya mbinu zinazotumika kupata pesa, na pia mambo muhimu unayopaswa kuyazingatia ili kufanikisha hilo.

Wengi wakiniuliza swali hili, huwa napata picha kwamba, wanahisi blogu ni kama kitu ambacho ukiwa nacho tu chenyewe kinafanya kazi hiyo ya kutengeza faida, na wengine hudhani, pengine walipotoshwa kuwa anaweza anzisha blogu na kuanza kupata pesa bila yeye kama mmiliki wa blogu kuweka juhudi zozote zile!, Hapana, tena ukiwa bloga mpya ndio inakuwa ni ngumu zaidi kupata faida, tazama orodha hii ndogo ya mambo ambayo unapaswa kufanya:

  1. Andaa na anzisha blogu yako
  2. Anza kuandaa na kuchapisha maudhui muhimu kwenye blogu yako
  3. Tafuta wasomaji na wafuatiliaji wa blogu yako
  4. Jenga mahusiano na ushiriki na wasomaji wa blogu yako
  5. Weka mifumo mbalimbali ya kupata pesa kupitia blogu yako

 

Unaona?, kupata pesa ni jambo la mwisho kabisa katika hatua hizo, ila kwa sababu ni hatua tano unaona ni kama rahisi sio?, nitazielezea zaidi hizo hatua ili upate kelewa juhudi unazotakiwa kuwekeza.

1. Andaa na anzisha blogu yako

Ndio, ni lazima uwe na blogu, na uwe unaimiliki wewe mwenyewe, inaweza kuwa rahisi kujifunza jinsi ya kuanzisha blogu kwa kusoma bandiko hili. ambalo ndilo limefanya niulizwe mswali mengi sana kuhusu faida.

2. Anza kuandaa na kuchapisha maudhui muhimu kwenye blogu yako

Blogu haina maana yeyote kama haina maudhui, maudhui(Content) ndio kitu pekee kitakacho tofautisha blogu yako na blogu zingine mtandaoni, maudhui ndio yatakayo kupatia wasomaji na wafuatiliaji wakudumu na hata wapya kwenye blogu yako.

Kimsingi hili ndio jambo la muhimu sana kuzingatia, mfano mwandishi wa habari ana nafasi nzuri ya kuwa na mudhui kwa sababu anakua na habari mpya kila mara, namna atakavyoziandaa habari zake na kuzichapisha kwa wakati inampa fursa kutumia blogu kuwafikia watu wengi kwa urahisi zaidi na wengi watapenda kuarifiwa punde tu unapochapisha habari mpya.

Chochote unachotaka kukizungumzia kwenye blogu yako chaweza kuwa ni kinalenga jamii fulani, au kundi fulani mfano watoto, vijana, wazee, wakulima, wanafunzi nakadhalika, jitahidi kiwe ni bora na chenye upekee. Maudhui mazuri na yenye muelekeo chanya yatawafanya wasomaji wako wajihisi kukufahamu na kukuamini sana hivyo kukuwekea mazingira bora zaidi ya kupata pesa baadae kupitia blogu yako.

3. Tafuta wasomaji na wafuatiliaji wa blogu yako

Blogu yako  ni mpya, hakuna mtu anaifahamu na unaamini una maudhui mazuri, sasa weka juhudi ya kuwapata wasomaji na wafuatiliaji, unatakiwa kuitangaza blogu yako. Muhimu hapa ni kujua ni watu gani (type of people) unaotaka wawe wasomaji na wafuatiliaji wa blogu yako. Kwa mfano umeandaa blogu ya mapishi!, ukishafahamu wasomaji wako ni watu wanaojihusisha na mambo ya mapishi basi fuatilia aina hii ya watu inaweza patikana wapi mtandaoni. Andaa orodha fupi yenye vitu kama:

  • Je!, wanafuatilia blogu zipi zingine zinazofanana au tofauti na maudhui ya blogu yako?
  • Wanashiriki kwenye majukwa gani mtandaoni? mfano (JamiiForums)
  • Kuna vipindi vya radio ama tv wanaweza kuwa wafuatilia pia?
  • Wanatumia mitandao ipi ya kijamii? orodhesha walau mitatu mikuu
  • Wanafuatlia watu gani kwenye hiyo mitandao ya kijamii?

 

Kwenye maeneo hayo utakayobainisha wasomaji unaowahitaji wanaweza kuwepo, wanaweza kuwa wanashiriki kwa kuchangia maoni na kulekezana. Hivyo na wewe inafaa uanze kuwa mshiriki wa maeneo hayo pia ili wakufahamu na pengine unaweza kutumia mwanya huo kuwajulisha na kuwakaribisha kuangalia blogu yako.

Muhimu ni kujenga uwepo wako, ufahamu, na kuchangia/kuongeza dhamani, epuka kuonekana kama mkorofi wa mtandaoni (spammy) kana kwamba unalazimisha watu wajue blogu yako tu, lakini wala huchangii mambo ya msingi wala kushauri.

Pia bila ushiriki wako, unaweza kuandaa bajeti ya matangazo na kutangaza blogu yako kwenye maeneo hayo ili ipate kufahamika.

4. Jenga mahusiano na ushiriki na wasomaji wa blogu yako

Kwa kuzingatia hizo hatua hapo juu, utakuwa na blogu nzuri, yenye maudhui sahihi na bila shaka umeanza kupata  wasomaji, sasa unapaswa kujenga mahusioano ya karibu na wasomaji wako ili waendelee kubaki na pia kukuletea wasomaji wapya.

Jibu maswali yao wanayouliza kuhusu mada husika kwa wingi kadri unavyoweza, pia wasiliana na baadhi yao wanapohitaji mawasiliano nawe kwa njia ya barua pepe nakadhalika.

Kushirikiana na wasomaji ni njia nzuri kukuwezesh akuapata pesa kupitia blogu yako.

5. Weka mifumo mbalimbali ya kupata pesa kupitia blogu yako

Sasa, umeshafanya yote yamsingi, lakini kupata pesa bado, na unahitaji kujaribu na kujuhudi njia mbalimbali kupata pesa. Bado safari ya kujifunza inaendelea, kuna njia nyingi sana za kupata pesa, ila hapa nitorodhesha chache ambazo mimi binafsi huwa nawashauri watu kuzitumia, tena ni njia ambazo bloga wengi huzitumia kupata pesa. Tuanze kujifunza njia hizi:

Kupata pesa kupitia matangazo ya CPC au CPM

Hii ni njia kuu ambayo hutumiwa sana na wamiliki blogu kupata pesa kwa kuweka matangazo madogo madogo kwenye kurasa za blogu zao, ziko aina mbili;

  • CPC/PPC – Cost per Click (au Pay Per Click), matanagazo ambayo yanakuwepo kwenye kurasa au pembeni mwa kurasa ya blogu yako yatakuingizia pesa kila msomaji atakapo gonga (click) tangazo hilo.
  • CPM – Cost per 1000 Impressions, yani kadiri tangazo litakavyoonekana mara nyingi katika nyakati tofauti tofauti na wasomaji tofauti tofauti utapata pesa kutoka kwa anayetangaza.

 

Google Adsense ndio mtandao maarufu wa kuchapisha na kupachika matangazo ya namna hii kwa wamiliki wa tovuti na blogu mbali mbali duniani, na inawalipa wamiliki wa blogu hizi vizuri kadiri blogu husika invyofaya vizuri kuzingatia hatua tulizojifunza awali, matangazo yanayopachikwa huteuliwa kielectroniki kuendana na maudhui, pia lugha ya blogu yako.

Uza matangazo binafsi

Ukiwa na watembeali wengi wa blogu yako kwa siku, sio lazima kutumia mitandao ya matangazo kama Google Adsense, Badala yake Makampuni yanaweza kukufuata moja kwa moja kutaka uwatangazie biashara zao. Unaweza pia kuwasiliana na wahusika moja kwa moja, na kwa kuwa hakuna mtu wa kati, hii inakuwezesha kuweka viwango unvyotaka kutoza kwa kila tangazo na ukapata faida kubwa zaidi.

Tangazo linaweza kuwa mfumo wa picha, video, an au hata chapisho zima kuhusu bidhaa fulani, nakadhalika.

Uza bidhaa za kidigitali

Ikiwa hutaki kuhangaika kutangazia watu wengine, unaweza kutumia blogu yako kutangaza na kuuza bidhaa za kidigitali mfano vitabu, picha, muziki, video n.k.

Unachotakwa kuzingatia hapa, bidhaa utakazoziuza ziandane na maudhui ya blogu yako na pia mahitaji ya wasomaji wako, hutakiwi kuacha kuandika mambo muhimu kwenye blogu yako na kufanya biashara tu, kumbuka watu wanafungu ablogu yako kujifunza, hivyo biashara iwe ni jambo la ziada ili wasomaji wako wasichukizwe na waendelee kufurahia blogu yako.

Andaa unachama wa kulipia kwenye blogu yako

Unaweza kuwa mbunifu zaidi na ukaandaa uanachama wa wasomaji wako ambao watajisajili na kulipia ili kupata huduma na maudhui ya kipekee zaidi, mfano mwandishi wa habari anaweza kuwalipisha wasomaji wake kupata habari mahususi zenye kuchambuliwa kwa kina na hata kushuhusia mahojiano aliyoandaa na baadhi ya watu mashuhuri.

Jenga jina na hadhi ya weledi wako

Blogu inaweza kuwa ni njia ya wewe binafsi kuonyesha uwezo na ufanisi ulionao katika fani mbalimbali na hivyo ukapata mialiko ya kufanya mafundisho, ama kupata kazi za kimikataba ambayo utakubaliana na wateja wako wakulipe.

 


Nimatumaini yangu nitakua nimejibu baadhi ya maswali kwenye chapisho hili, tadhali usiache kujifunza na kuuliza kama una swali jingine, nami nitakuwa huru kukujibu bila shaka.

Nitanendelea kushirikisha taarifa muhimu na mbinu mbali mbali zinazohusu TEHAMA kwa ujumla, hivyo shirikisha bandiko hili na mengine mengi ili nipate wasomaji wengi zaidi kama wewe na hatimae kuongeza ufahamu wa mambo haya katika jamii yetu.

Tumia program za Windows kwenye Linux!

Linux ni moja kati ya mifumo mashuhuri ya uendeshaji kompyuta, imekua ikitumika tangu miaka ya 1984. Programu hii hupatikana bure kabisa na katika ladha tofauti zinazofahamika kama ditros, kati ya distro maarufu sana duniani ni Ubuntu, Linux Mint, na fedora. Tofauti na Windows au Mac za Apple, kwenye Linux programu zote waweza pata bure pia bila gharama yoyote.

Ingawa ni ya bure, Umaarufu wa Linux pia hutokana na uwezo wake wakutosumbuliwa na virusi (Computer Viruses) kama ilivyo kwenye Microsoft Windows, na uwezekano wa kupata msaada kwenye mtandao kwa urahisi na haraka sana.

Changamoto kubwa kwa wanaoanza ama kuhamia kutoka kwenye Windows na kuanza kutumia Linux, hasa Ubuntu, huwa ni kuzoea muonekano, na zaidi ni kupata programu (Softwares) ambazo alikuwa anazitumia kwenye Windows. Mfano, programu ya Kuchapa (Microsoft Word) na nyinginezo nyingi. Kwenye Linux kuna programu Mbadala ya zile zilizoko kwenye Windows, hata hivyo zinaweza zisifikie kiwango na ubora wa zile za kwenye Windows, lakini kwa kiasi kikubwa zinaweza kukusaidia kufanya unayohitaji kama ambayo ungefanya kwenye windows. Mifano ya programu mbadala zilizoko tayari ndani ya ubuntu ni kama ifuatavyo:-

  • Mozilla Firefox – kuperuzi wavuti, waweza pia kuingiza google chrome
  • Libre Office – mbadala wa Microsoft Office
  • Mozilla Thunderbird – mbadala wa Microsoft Outlook
  • Document Viewer – Mbadala wa Adobe reader
  • Rythimbox Music Player
  • Videos Media Player

 

Nitazungumzia namna mbalimbali ambazo unaweza kuzitumia kwenye linux kufanya kama ambavyo unhgefanya kwenye windows. Njia hizi baadhi zaweza kukusaidia pia hata ikitokea umeenda sehemu na ukakuta kompyuta inatumia mifumo wa linux badala ya windows uliyozoea mfano kwenye Internet Cafe.

1 : Tafuta mbadala wa programu.

Kuna tovuti maarufu sana inaitwa osalt.com, tovuti hii inakuonyesha programu mbadala wa programu nyingi ambazo zinauzwa. Mibadala hii si kwa ajili ya Linux/Ubuntu peke yake, yaweza pia kutumia kwenye Windows, Mfano Ukitaka mbadala wa Microsoft Word, utakuta kuna nyingi ikiwemo, AbiWord, OpenOffice Writer, KWord n.k.

2 : Tumia programu za online

Siku hizi kumeibuka teknolojia ya Cloud Computing ambayo inawezesha mtumiaji wa kumpyuta kutojali kuwa na kifaa fulani tu ili kuona na kufanya kazi zake. Cloud Computing inasaidia pia kushirikiana na wenzako na huna haja ya kubeba kompyuta tena kama unasafiri, ili mradi unakoenda kuwe na kompyuta na mtandao. Hivyo kuna huduma nyingi mtandaoni zinazowezesha wewe kuhifadhi mafaili yako ikiwemo nyaraka, picha, miziki na hata video na ukaweza kuvipata katika vifaa vingi tofauti.

Kwa njia hii unaweza kutumia linux na ukiwa na mtandao basi utachapa barua zako ikiwa online, baadhi ya huduma za bure unazoweza kutumia ni kama:-

  1. Google Drive kuhifadhi mafaili na Google Docs kama mbadala wa Microsoft Office
  2. Drop Box kuhifadhi mafaili yako ya aina zote.
  3. Office Online hii ndio kila kitu kama cha Microsoft Office ila ni online
  4. PIXLR hii ni kwa wale wanotumia photoshop na programu za graphics.

 

Kwa kila ain aya programu, ina mpbadala wake kwenye wovuti, hivyo ni wewe kutafuta tu.

3 : Sanikisha programu kwa kutumia WINE au PlayOnLinux.

Kuna programu inaitwa WINE ikimaanisha “Wine is not Emulator” ambayo inakuwezesha kusanikisha(Install) programu za Windows moja kwa moja kama vile iko kwenye Windows. Programu hii unaweza kuitafuta ndani ya Ubuntu kwa jina la Wine au PlayOnLinux. Ukishakuwa nayo unaweza kusanikisha baadhi ya programu muhimu kama Microsoft Office, Adobe Photoshop, na nyininezo nyingi.

4 : Sanikisha Windows kwenye Virtual Machine

Kwa kuwa Linux/Ubuntu inahakikisha usalama zaidi dhidi ya virusi vya kompyuta, na iko haraka kuliko Windows, unaweza pia ukaingiza Windows ndani ya Ubuntu kwa kutumia programu maalumu inayoitwa Virtual Box. Virtual Box inaweza kutengeza mfano wa kompyuta nyingine (Virtual Machine) ndani ya kompyuta yako uliyonayo, halafu ukaingiza windows na ukatumia programu zako unazotaka endapo njia nilizoordhesha hapo juu hazikufaa.

ZINGATIA: Hatua hii ya kutumia Virtual Box waweza pia kuifanya ndani ya Windows na ukasanikisha ubuntu ili kuijaribu na kujifunza kabla haujaamua kuitumia rasmi.

Bila shaka umeweza kupata angalau uelewa wa namya kutumia baadhi ya programu uzipendazo kwenye Windows ndani ya Linux. Kwa maoni, maswali na ama ushauri usisite kuniandikia kwenye fomu ya maoni hapo chini, ama kutuma ujumbe wako kwenda info@webnerdtz.com

VIDEO: Tumia Windows kwa Kiswahili

Habari, Je!, wewe ni mpenzi wa lugha ya kiswahili?, na ungependa kutumia kompyuta yako au kifaa cha cha windows kikiwa na lugha hiyo?. Mikrosoft windows ana kifurushi cha lugha yetu pendwa na kinaweza kutumika kwenye kompyuta yako.

Kwenye makala hii nitakuonyesha namna unaweza kufanya kompyuta yako yenye Windows 8 ambayo pia inafanana na baadhi ya vifaa vya Windows Mobile iwe kwa lugha ya kiswahili, na hata lugha nyingine pia kama utapenda, namna ya kufanya hivyo hakutofautiani sana.

Utahitaji kuwa mtandaoni na kifaa chako, ili uweze kupakua kabrasha la lugha, ba baada ya kuingiza lugha kama utakavyoona, itabidi utoke (sign out/logout) na uingie tena(sign in/login) ili kuona mabadiliko ya lugha kwenye kifaa chako.

Angalia video hii hapa chini kujifunza.

Jinsi ya kusanikisha Movie Maker kwenye Windows 8

Habari wadau, ni muda sasa umekwenda lakini si mbaya leo tukijifunza kitu pia. Umewahi kujiuliza Video zinafanyiwa vipi editing?. Kama ndio bila shaka umeshafahamu kuwa Editing inafanyika zaidi kwenye Computer, na kuna programs au software ambazo nyingi ni ghali kuzinunua ambazo zitakuwezesha kufanya jambo hilo.

Kabla hatujazifahamu programu zinazotumika kwa shughuli hiyo, kwanza tujifahamishe kuhusu sifa zake za msingi. Programu ya Editing inategemewa kukuwezesha mtumiaji kufanya mambo yafuatayo:

  • Kuweza kufanyia kazi aina tofauti za mafaili utakayokuwa nayo, na kuweza kuyabadili mafaili hayo kwenda kwenye mfumo mwingine; aina za mafaili ni kama avi,mp4,mpg,jpg png,mp3 n.k
  • Kuunganisha vipande vya video, kukata sehemeu za video ambazo hutaki ziwepo na kuziondoa,
  • Kufanya angalau baadhi ya marekebisho kwenye sauti ya video ikiwa ni pamoja na kuongeza sauti ya ziada kama voice-over, athari za sauti na muziki wa nyuma kwenye video hiyo
  • Kufanya angalau marekebisho ya muonekano wa video husika, kama vile mwanga n.k, hapa tunazunguzia filters na effects mbalimbali ambazo zitapendezesha video yako machoni kwa watazamaji.
  • Kuwa na uwezo wa kuongeza mabadiliko kati ya sehemu za video zilizo katika mtiririko wa hadithi mfano picha kufifia, kupunguzwa, unafifia na nyeusi, unafifia na nyeupe n.k.
  • Kuwa na uwezo wa kuongeza maneno na vijimaneno kwa udhibiti mzuri na makala aina mbalimbali kwa ubunifu.

Hizi ni sifa za msingi kuwa nazo katika programu ya kurekeishia video zako. Hivyo kama una kamera nzuri inayoweza kurekodi video safi na una kompyuta nyumbani bila shaka utatamani kutumia programu hizi ili kupunguza gharama, maana waweza rekebisha video zako na kuzichoma kwenye CD na ukahifadhi kumbukumbu zako kisasa zaidi, au sio?.

Kwa ujumla ziko programu nyingi maarufu, na kama nilivyokwisha bainisha awali ni kuwa nyingi kati ya hizo zinauzwa na zina mambo mengi ya ziada ambayo si ya lazima sana kuwa nayo kwa video zako za nyumbani, hivyo Microsoft Windows huwa inawapatia watumiaji wake programu ambayo ni bure na inakuwezesha kufanya yote ya msingi.

Programu hii inaitwa Windows Movie Maker na kwa bahati mbaya inaweza isiwepo kwenye baadhi ya kompyuta zenye programu endeshi ya windows. Kama haipo kwenye kompyuta yako pia nenda hapa kuipakua kulingana na toleo la Windows yako. Utaipakua na kisha kuisanikisha kwa kufuata maelekezo yake.

Ukiifungua programu hiyo itaonekana hivi:

mm

Movie Maker Ikifunguka

Ni matumaini yangu utaweza kujifunza zaidi jinsi ya kuitumia programu hiyo kwa iko rahisi na vitu vyake viko wazi sana kuielewa, na pengine waweza kuja kuwa editor mzuri zaidi hata ukapata hamu ya kutumi programu kubwa za aina hii.

Endelea kufurahia kompyuta yako.

Usiogope kufungua tovuti sababu ya utofauti wa Lugha!

Ndio, nafahamu kuwa tovuti nyingi zina lugha za kigeni, tena tovuti hizi mara nyingi ndio zenye tija hasa!, lakini watumiaji wa kitanzania walio wengi wanafahamu kingeereza pia, vipi sasa wakikuta tovuti ina lugha ya kifaransa ama kireno, au kichina kabisa?, Kwa harak haraka mtu huyu atafunga tu huo ukurasa na kuperuzi kurasa zingine!

Usiogope, unaifahamu GOOGLE sio?, basi ni rahisi sana, google wana kifaa murua sana unachoweza kukitumia ili kuweza kutafsiri, sio tu tovuti nzima bali hata neno mojamoja. Ni rahisi sana wewe kwenye kivinjari (Browser) chako andika anuani hii http://translate.google.com waweza kubonyeza hapa pia. Ukurasa kama huu hapo chini utafunguka, chakufanya andika neno ambalo unataka litafsiriwe upande wa kushoto halafu chagua lugha ya tafsiri upande wa kulia na utaona tafsiri yake.

Ikiwa kuna tovuti ungependa itafsiriwe waweza kuandika anuani ya tovuti hiyo mfano http://www.france.fr/ upande wa kulia itatokea neno hilohilo kama kiungo, basi bonyeza(click) kiungo hicho na utaona ukurasa huo unafunguka kwenye lugha ya tafsiri.

Waweza pia kukopi na kupesti ukipenda ili kuona tafsiri.

DONDOO: Unaweza andika hadithi yako ya kiswahili ambayo wataka iwe kwa kingereza kwa kutumia kifaa hichi kwa urahisi sana!, nimekuwa nikijaribu kufanya hivyo mara nyingi sana kipindi nipo shuleni!.

Bila shaka kifaa hichi cha mtandaoni kitakuwia manufaa sana. Waweza pia kutazama video hii kujifunza zaidi:

Orodha ya maneno ya TEHAMA na tafsiri zake!…

Habari!, najua kwa sasa Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano inashika hatamu nchini mwetu na hii inafanya watu wengi wapende kutumia vifaa kama kompyuta na simu za mkonnoni ili wasiwe nyuma. Pamoja na hayo bado kuna ugumu wa kutumia na kufurahia teknolojia hii, achilia mbali athari ambatanishi zinazoweza kusababishwa na kutokuelewa lugha inayotumika ambayo ni kiingereza, pia hata kiswahili chake kinaonekana kuwa kigumu sana kwa watumiaji wapya na hata wale ambao walishazoea kutumia kompyuta kwa kiingereza.

Mimi kama mdau wa TEHAMA inchini bado nina hamu ya kuona Watanzania wenzangu wakuwa huru na kujivunia kutumia kompyuta kwa lugha yao kama wanavyotumia wenzetu.

Kuna faida nyingi sana ukijaribu kutadhmini hili. hata hivyo ugumu wa kiswahilli chenyewe kiapelekea hata waandaaji wa programu za kompyuta kushindwa kuweka maneno sahihi na marahisi kwenye programu zao. Mfano neno password ambalo kwa tafsiri halisi ni neno ambalo mtumiaji atatakiwa kuliandika kabla hajapata ruhusa ya kufanya jambo fulani katika mfumo wa kikompyuta limekuwa na tafsiri mbili kinzani ambapo mwisho wa siku mtumiaji ataamua kusema password ni nenosiri, wakati wanazuoni wanasisitiza kuwa password tafsiri yake ni nywila, sasa wangapi kati yetu tulikuwa tunalifahamu neno hili?

Bila kukuchosha, ningependa upakue faili hili na upate kufahamu baadhi ya maneno ya tehama na tafsiri zake. Maneno hayo yanaweza kuwa rejea yako endapo utahitaji kufahamu zaidi neno fulani pindi ukikutana nalo.

Bofya hap Kupakua Faili lenye Orodha ya maneno

© 2024, WEBNERD SOLUTIONS