Kompyuta ni nini?

Umeanza kutumia kompyuta?, je una maswali unaposikia watu wanasema maneno na misamiati ya kompyuta na ukashindwa kuelewa?, bas makala hii itajadili mada yenye kutambulisha kwako mambo muhimu yanayohusu kompyuta. Usiwe na hofu, kwa sababu tulipofikia kwa sasa hatuwezi kukwepa kutumia kompyuta, hivyo ukiwa na uelewa kidogo tu utakaojifunza hapa, utafahamu kompyuta ni nini na utabaini aina mbali mbali za kompyuta zilizopo. haya tuanze kujifunza. Kompyuta ni nini?

Kompyuta ni kifaa cha ki elektroniki ambacho hufanya kazi kwa kuendesha taarifa, au data. Kifaa hichi kina uwezo wa kuhifadhi, kuchambua, na kuchakata data/taarifa. Bila shaka unafahamu kuwa waweza tumia kompyuta kuchapa nyaraka mbalimbali, kutuma barua pepe, kucheza michezo, na kuvinjari mtandaoni. Waweza pia kutumia kompyuta kuhariri picha, video na mambo mengine mengi. Tafadhali angalia picha hii hapa chini kuona watu mbali mbali wakitumia kompyuta (Picha hii nimeitoa mtandaoni kwanuani hii).

computer_grid

Vifaa na Programu za Kompyuta.

Kabla hatujajifunza aina za kompyuta, tujifunze vitu/mambo muhimu yanayokamilisha kompyuta. Kumpyuta ina sehemu kuu mbili, Vifaa ( Hardware ) na Programu (Software).

Vifaa(Hardware) vinashikika na ndio vinaunda mifumo ya ki elekroniki ambayo inaonekana kifizikia mfano, kipanya(mouse), kiambaa (keyboard), Kioo cha kuangalizia (Monitor/screen) na vyote vilivyomo ndani ya kasha la kompyuta.

Programu(Software) hazishikiki, ni mkinyaiko wa maelekezo ya kuviongoza vifaa vifanye kazi na kusababish amatokeo ambyo mtumiaji anataka yatokee kwenye kila jambo. Mfano wa programu ni kivinjari cha wavuti  (web browser) au programu ya kuandika nyaraka ya Microsoft Word, na zingine nyingi ambazo tutajifunza huko mbele. Kimsingi hizi programuu ndizo zinazofanya watu wafurahie na wanufaike kutumia kompyuta lakini zitafanya yote juu ya vifaa vyenye uwezo wa kupokea maelekezo hayo.

Chochote unachofanya kwenye kompyuta hutegema vifaa na programu. Mfano hivi sasa yawezekana unasoma makala hii kwa kutumia kivinjari (web browser) ikiwa ndani ya kompyuta ya mezani, na unatumia kipanya(mouse) kubofya viungo vilivyomo kwenye kurasa ili kufungua kurasa zingine kwenye tovuti hui au nyinginezo. Na baada ya kujifunza aina za kumpyuta utajiuliza kwenye aina tofauti za kompyuta hizo ni vifaa gani vinaweza kutumika kama kipanya.

Aina za kompyuta

Wengi wanaposikia kompyuta huelekeza mawazo yao kwenye kompyuta za mezani (Desktop Computers) au kompyuta za mpakato (Laptop Computers), lakini ukweli ni kwamba kuna aina nyingi za kompyuta zaidi ya hizo mbili nilizokwisha zitaja hapa. Na kwa maendeleo ya tekinolojia yalipofikia hivi sasa, ni muhimu ukafahamu kuwa kompyuta zimetuzunguka kila mahali, ziko mezani, mikononi, barabarani, hospitali, na kila mahali.

Kimsingi kompyuta zimegawanyika katika makundi makuu mawili, kuna kompyuta za madhumuni ya jumla (General purpose computers) hizi ndio wengi wanazitambua na kuzibainisha moja kwa moja kama kompyuta, lakini pia ziko kompyuta za kusudi maalumu (Special purpose computers) mfano, kikokotozi (calculator) ni kompyuta kwa ajili ya kukokotoa tu. Vifaa vingi vya eletroniki mfano luninga (TV), Saa za digitali (digital watches), kisimbuzi (decoders), simu za mkononi za kawaida (feature phones) zina kompyuta maalumu kwa kazi yake, na zina uwezo wa kuhifadhi, kuchakata, na kuendesha data kulingana na mipaka yake.

Tujifunze sasa baadhi ya kompyuta ambazo wengi huzibainisha moja kwa moja, mada yakuelekeza aina zote za kumpyuta na zinavyofanya kazi iko inje ya makala hii, badala yake tutaangazia zaidi kompyuta zinazotumiwa na watu binafsi zaidi (personal computers), kama zifuatavyo.

Kompyuta ya mezani (Desktop Computer)

Hizi utazikuta sana maofisini, majumbani, mashuleni nakadhalika, zinakaa juu ya meza, zaweza kuwa ndogo, saizi ya kati, au kubwa sana kimuonekano lakini umbile sio lazima lishabihiane na uwezo, tutakuja kujifunza sifa zinazoipa uwezo kompyuta kwenye makala nyingine. Mara nyingi iko pembeni ya Kioo cha kungalizia (monitor) , pia imeunganishwa na kipanya (mouse), na kiambaa (keyboard).desktop-computer1

Konpyuta ya mezani ni rahisi kuiboresha kwa kuongezea vitu, na pia bei yake ni rahisi kwa sababu vifaa vyake hutengezwa kwa maumbile makubwa kiasi ambvyo kitekinolojia sio ghali kuvitengeneza ukilinganisha na vifaa vya kompyuta ndogo kiumbo. Uliknganisha kumpyuta ya mezani na ya mpakato zenye uwezo sawa, utakuta ya mezani ni ya gharama nafuu sana kwa bei.

Kompyuta ya kupakata (Laptop computer)

Hii ni aina ya pili maarufu ya kompyuta binafsi, ni ndogo na zinabebekam hivyo waweza kuzitumia karibu kila mahali uendapo kwa sababu zinatumia betri ya kuchaji. Mara zinatuza chaji kwa muda zaidi ya masaa mawili, hivyo wengi wanafurahia kuzitumia kwa uhuru wa kuweza kutembea nazo. Lenovo-Notebook-İndirimi1

Kutokana na udogo wake sio rahisi sana kuziongezea au kubadilisha vifaa vyake vya ndani kama ambvyo ungefanya kwenye kompyuta za mezani, inagawa inawezekana, alini huwa zimetengezwa na sifa zenye kuifaa ikiwa hivyo, labda itokee kifaa kimeharibika.

Kipanya na kiambaa ni sehemu ya kompyuta hii, ila pia waweza kuunga vifaa vya pembeni endapo utahitaji.

 

Kompyuta Kibao (Tablet computer)

Kompyuta kibao ni kompyuta ndogo zaidi ya kompyuta mpakato, yenyewe ni ya kushika mhononi tu, na rahisi zaidi kutembea nayo popote, na huwa zikikaa na chaji kuliko za kupakata. Badala yakutumia kipanya na kiambaa, yenyewe unagusa na vidole vyako kwenye kioo ili kuandika au kuperuzi, pia zingine huwa na kalamu maalumu (Stylus) unayoweza kuchora au kuandika juu ya kioo chake. iPad ni mfano wa kompyuta maaarufu ya namna hii.Apple-tablet-computer-con-001

Kompyuta hizi, hafinayi kila kitu ambacho ya mezani au ya kupakata yaweza fanya, lakini waweza kuitumia kama unataka kujisomea, kucheza michezo, kuwasiliana na watu kwenye mitandao ya kijamii, kusoma barua pepe, na kujiburudisha kwa kusikiliza miziki na kuangalia video. Kutokana na muundo na malengo ya matumizi yake, hazina uwezo mkubwa wa kuhifadhi na kuchakata data, na utaifurahia zaidi kama utakuwa na mtandao wa wavuti(internet), kwa mtu mwenye kuihitaji burudani na kupata taarifa kwa urahisi popote alipo, kompyuta hizi huwafaa sana, lakini bado utahitaji kuwa na ya mezani au ya kupakata ili uweze kufanya kazi zingine za kompyuta kama kuchapa nyaraka n.k.

Seva kompyuta (Server)

Seva ni kompyuta ambayo inahudumia kompyuta zingine zilizo kwenye mtandao, mtandao unaweza kuwa wa ndani ya ofisi (local area network), au mtandao wa wavuti (internet). Makampuni mengi yanatumia seva kuifadhi mafaili na kutoa huduma zigine kwa wafanyakazi na pia kitoa taarifa kwa wateja mbalimbali. Seva yaweza kuonekana kama kama kompyuta ya kawaida au yenye umbile kubwa zaidi, na kwenye makampuni makubwa seva hutengawa kwenye vyumba maalumu na hutunzwa kwa mumakini mkubwa kwa sababu zintegemewa na mamilioni ya wahiyajio huduma.computer-servers

Seva ndio mchezaji mkuu wa mtandao, ndio wanaofanya watu kuwa na tovuti duniani, na ndio vichochezi vya tekinolojia ya wingu la makompyuta (cloud computing). Unapoangalia muziki kwenye tovuti ya www.youtube.com video zote hizo zimehifadhiwa kwenye seva, na seva inakuhudumia video unayotaka kuiona kwenye kompyuta yako, ba inafanya hivyo kwa ziadi ya kompyuta milioni kwa wakati mmoja, hivyo seva zina uwezo mkubwa sana wa kuhifadhi na kuchakata data, na ni gharama kuziunda, na kuzitunza pia.

 

 

Aina nyigine za kompyuta

Kama nilivyogusia awali, leo hii kuna aina lukuki za kompyuta ambazo kwa kiasi kikubwa ni za matumizi maalumu. Ili kuongezea elimu yetu hii, nitaorodhesha baadhi ya kompyuta hizo:-

  1. Simu za mikononi – wengi wanatumia simu za mikononi za kisasa (Smartphones) kufanya mambo mengi amabyo ungeweza kufanya kwenye kompyuta ya mezani kama kucheza michezo (games), kusom abarua pepe, na kuangalia mztandao pia kuwasiliana na marafiki kwenye mitandao ya kijamii
  2. Kumpyuta za michezo (Game consoles) – mfano playstation, nintendo n.k, hizi ni kompyuta maalumu kwa michezo ya kwenye luninga, mfano mpira, magari n.k.
  3. Luninga (TV) – hizi za kisasa zinauwezo wa kuunganisha kwenye mtandao wa wavuti na kufungua taarifa mbali mbali

Hitimisho

Tumejifunza kompyuta ni nini?, na watu hutumia kompyuta kufanya mambo gani, pia tumeona baadhi ya aina mbali mabli za kompyuta na kufahamu matumizi yake na mipaka yake kwa ujumla. Somo hili halitaishia hapa kwani bado kuna mengi ya kujifunza kuhusu kompyuta hizi, kwenye makala nyingine tutajifunza kuhusu uwezo wa kumpyuta na unaweza vipi kufahamu, pia sifa za programu endeshi za kompyuta hizo.

Tafadhali anedela kufungua tovuti hii ili uweze kujifunza zaidi kuhusu mambo ya TEHAMA.

© 2024, WEBNERD SOLUTIONS