+255 717 074797   bbk@webnerdtz.com

VIDEO: Tumia Windows kwa Kiswahili

Habari, Je!, wewe ni mpenzi wa lugha ya kiswahili?, na ungependa kutumia kompyuta yako au kifaa cha cha windows kikiwa na lugha hiyo?. Mikrosoft windows ana kifurushi cha lugha yetu pendwa na kinaweza kutumika kwenye kompyuta yako. Kwenye makala hii nitakuonyesha namna unaweza kufanya kompyuta yako yenye Windows 8 ambayo pia inafanana na baadhi ya […]

Habari, Je!, wewe ni mpenzi wa lugha ya kiswahili?, na ungependa kutumia kompyuta yako au kifaa cha cha windows kikiwa na lugha hiyo?. Mikrosoft windows ana kifurushi cha lugha yetu pendwa na kinaweza kutumika kwenye kompyuta yako.

Kwenye makala hii nitakuonyesha namna unaweza kufanya kompyuta yako yenye Windows 8 ambayo pia inafanana na baadhi ya vifaa vya Windows Mobile iwe kwa lugha ya kiswahili, na hata lugha nyingine pia kama utapenda, namna ya kufanya hivyo hakutofautiani sana.

Utahitaji kuwa mtandaoni na kifaa chako, ili uweze kupakua kabrasha la lugha, ba baada ya kuingiza lugha kama utakavyoona, itabidi utoke (sign out/logout) na uingie tena(sign in/login) ili kuona mabadiliko ya lugha kwenye kifaa chako.

Angalia video hii hapa chini kujifunza.

Usiogope kufungua tovuti sababu ya utofauti wa Lugha!

Ndio, nafahamu kuwa tovuti nyingi zina lugha za kigeni, tena tovuti hizi mara nyingi ndio zenye tija hasa!, lakini watumiaji wa kitanzania walio wengi wanafahamu kingeereza pia, vipi sasa wakikuta tovuti ina lugha ya kifaransa ama kireno, au kichina kabisa?, Kwa harak haraka mtu huyu atafunga tu huo ukurasa na kuperuzi kurasa zingine! Usiogope, unaifahamu […]

Ndio, nafahamu kuwa tovuti nyingi zina lugha za kigeni, tena tovuti hizi mara nyingi ndio zenye tija hasa!, lakini watumiaji wa kitanzania walio wengi wanafahamu kingeereza pia, vipi sasa wakikuta tovuti ina lugha ya kifaransa ama kireno, au kichina kabisa?, Kwa harak haraka mtu huyu atafunga tu huo ukurasa na kuperuzi kurasa zingine!

Usiogope, unaifahamu GOOGLE sio?, basi ni rahisi sana, google wana kifaa murua sana unachoweza kukitumia ili kuweza kutafsiri, sio tu tovuti nzima bali hata neno mojamoja. Ni rahisi sana wewe kwenye kivinjari (Browser) chako andika anuani hii http://translate.google.com waweza kubonyeza hapa pia. Ukurasa kama huu hapo chini utafunguka, chakufanya andika neno ambalo unataka litafsiriwe upande wa kushoto halafu chagua lugha ya tafsiri upande wa kulia na utaona tafsiri yake.

Ikiwa kuna tovuti ungependa itafsiriwe waweza kuandika anuani ya tovuti hiyo mfano http://www.france.fr/ upande wa kulia itatokea neno hilohilo kama kiungo, basi bonyeza(click) kiungo hicho na utaona ukurasa huo unafunguka kwenye lugha ya tafsiri.

Waweza pia kukopi na kupesti ukipenda ili kuona tafsiri.

DONDOO: Unaweza andika hadithi yako ya kiswahili ambayo wataka iwe kwa kingereza kwa kutumia kifaa hichi kwa urahisi sana!, nimekuwa nikijaribu kufanya hivyo mara nyingi sana kipindi nipo shuleni!.

Bila shaka kifaa hichi cha mtandaoni kitakuwia manufaa sana. Waweza pia kutazama video hii kujifunza zaidi:

Orodha ya maneno ya TEHAMA na tafsiri zake!…

Habari!, najua kwa sasa Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano inashika hatamu nchini mwetu na hii inafanya watu wengi wapende kutumia vifaa kama kompyuta na simu za mkonnoni ili wasiwe nyuma. Pamoja na hayo bado kuna ugumu wa kutumia na kufurahia teknolojia hii, achilia mbali athari ambatanishi zinazoweza kusababishwa na kutokuelewa lugha inayotumika ambayo ni kiingereza, […]

Habari!, najua kwa sasa Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano inashika hatamu nchini mwetu na hii inafanya watu wengi wapende kutumia vifaa kama kompyuta na simu za mkonnoni ili wasiwe nyuma. Pamoja na hayo bado kuna ugumu wa kutumia na kufurahia teknolojia hii, achilia mbali athari ambatanishi zinazoweza kusababishwa na kutokuelewa lugha inayotumika ambayo ni kiingereza, pia hata kiswahili chake kinaonekana kuwa kigumu sana kwa watumiaji wapya na hata wale ambao walishazoea kutumia kompyuta kwa kiingereza.

Mimi kama mdau wa TEHAMA inchini bado nina hamu ya kuona Watanzania wenzangu wakuwa huru na kujivunia kutumia kompyuta kwa lugha yao kama wanavyotumia wenzetu.

Kuna faida nyingi sana ukijaribu kutadhmini hili. hata hivyo ugumu wa kiswahilli chenyewe kiapelekea hata waandaaji wa programu za kompyuta kushindwa kuweka maneno sahihi na marahisi kwenye programu zao. Mfano neno password ambalo kwa tafsiri halisi ni neno ambalo mtumiaji atatakiwa kuliandika kabla hajapata ruhusa ya kufanya jambo fulani katika mfumo wa kikompyuta limekuwa na tafsiri mbili kinzani ambapo mwisho wa siku mtumiaji ataamua kusema password ni nenosiri, wakati wanazuoni wanasisitiza kuwa password tafsiri yake ni nywila, sasa wangapi kati yetu tulikuwa tunalifahamu neno hili?

Bila kukuchosha, ningependa upakue faili hili na upate kufahamu baadhi ya maneno ya tehama na tafsiri zake. Maneno hayo yanaweza kuwa rejea yako endapo utahitaji kufahamu zaidi neno fulani pindi ukikutana nalo.

Bofya hap Kupakua Faili lenye Orodha ya maneno