Mfumo wa uendeshaji kompyuta

Mfumo wa uendeshaji kompyuta (Computer Operating System) ama waweza kuita mfumo endeshi ya kompyuta ndio programu muhimu inayowezesha kompyuta kufanya kazi. Mfumo huu ndio unasimamia vifaa vyote kwenye kompyuta na kuwezesha programu zingine kutumia vifaa hivyo kutimiza kazi inayopaswa kufanya. Inasimamia kumbukumbu, michakato na kila kitu cha kukurahisishia wewe mtumiaji kuwasiliana na kompyuta pasi na kufahamu lugha yake. Bila mfumo huu, kompyuta haina maana, na isingeweza kuonekana kifaa matata kama kinavyoheshimika, ni mfumo huu wa endeshaji haswa ndio kila kitu.

Kazi kuu ya mfumo endeshi wa kompyuta

Mfumo huu unawajibu wa kusimamia vifaa vyote vilivyopo kwenye kompyuta, kuhakikisha kila programu zilizofunguliwa na zitakazofunguliwa zinapata nafasi ya kutumia vifaa kwa uwiano ulio sawa. Programu hii pia ina hakikisha wewe mtumiaji unaweza kuwasiliana na kompyuta kwa kukupatia njia ya kuitumia (interface), mfano wengi tumeozoea kuona mshale wa kapuku(mouse) na ikoni vya kubonyeza ili kufungua au kufunga dirisha(window) la programu kwenye kompyuta, Ama wengine kompyuta zao huzipa sehemu ya kuandika amri(commands) za kuifanya kompyuta ifanye kazi fulani.

Aina za mifumo endeshi ya kompyuta

Kompyuta nyingi za watumiaji wa kawaida huuzwa zikiwa na mfumo endeshi tayari, hata hivyo unaweza kubadilisha au kuboresha(upgrade) mfumo endeshi uliomo. Kati ya mifumo endeshi maarufu kwenye kompyuta binafsi ni Microsoft Windows, Linux, na Apple Mac OS X. Mifumo hii ya kisasa ni yenye kutumia muonekano unaofahamika kama Graphical User Interface (GUI) ikimanisha muonekano wenye grafiki ambao unakuwezesha kutumia kipanya kubofya ikoni(icons), menyu, na matini(text).

Kila mfumo endeshi unamuonekano na ladha yake, ingawa ina fanania na zote zimefanywa kuwa rahisi kutumia, lakini ukibadili kutoka mfumo endeshi mfano wa Windows kwenda wa Linux kama ubuntu utaweza kupata tabu kidogo mpaka uzoee munekano huo kwa muda kidogo.  Kabla y amuonekano wa grafiki, kompyuta zilikuwa zikitumia muonekano wa giza tu na kupwatia mtumiaji mstari wa amri (Command Line Interface), hivyo mtumiaji alipaswa kuandika kila kitu kwa kutumia kibodi tu, hakuna kubofya kwa puku (Mouse).

Mirosoft Windows

Mfumo huu umetengezwa na kampuni ya Microsoft kati kati ya mwaka 1980, na tangu kuanza kwake, Windows imekua na mateoleo mbali mbali yenye kuakizi kukua kwa tekinolojia na ubora wake.

Ni Programu endeshi maarufu sana duniani, na toleo la hivi karibuni ni Windows 10, ya nyuma yake ni Windows 8, Windows 7, na Windows Vista. Pamoja na matoleo hayo pia utataka kujua kama Windows hiyo ni kwa matumizi ya Nyumani (Home Edition), Mabigwa (Professional Edition), au Mwisho (Ultimate Edition), ni muhimu ukafuatilia haya ili ujiridhishe kulingana na matumizi yako.

understandos_windows

Muonekano wa Mikrosoft Windows 7

Mac OS X

Mfumo endeshi huu umetengezwa na kampuni inayotwa Apple Inc., moja ya makampuni maarufu kutokana na bidhaa zake kuwa za ghali, na za kipekee, zina mionekano mzuri sana ukilinganisha na Programu Endeshi zingine. Kulingana na takwimu za matumizi kutoka statcounter.com 2016, OS X ina 9% ukilinganisha na Windows ambayo ina zaidi ya 50%. (angalia futiko la takwimu mwisho wa makala hii)

understandos_os_x

Muonekano wa Mac OS X

 

Linux

Linux ni mfumo endeshi ambao hufanywa kama programu za chanzo huria (open source), watu na makampuni mbali mbali duniani hutenegeneza ladha tofauti juu ya programu endeshi ya linux, hivyo hakuna kampuni maalumu kama ilivyo Microsoft kwa Windows au Apple kwa Mac OS X. DistroWatch.com. inaorodhesha mateleo takiribani 100 ya Linux, ambapo matoleo maarufu zaidi ni Ubuntu, Mint, na Fedora.

FHv2w

Muonekano wa Ubuntu

Mifumo endeshi ya vifaa vya mkononi

Vifaa vya mkononi kama simu hasa za kisasa, kompyuta kibao (Tablets) na kadhalika, havitumii programu endeshi kama hizo tulizoziona hpo juu, zenyewe hutumia programu endeshi maalumu kwa ajili ya kifaa hicho, na hazina uwezo wa kufanya kila kitu kama hizi zingine. Mafano wa programu endeshi maarufu kwa simu ni Google Android, Apple iOS, na Windows Mobile.

Hitimisho

Leo umepata kufahamu mifumo endeshi maarufu ya kompyuta, na jinsi gani mifumo hiyo iko maarufu kwa watumiaji duniani. Kwenye makala zinginezo utapata kujifunza namna ya kufanya mambo mbali mbali ikiwa kompyuta yako una mfumo mmoja wapo ya hio. Nakucha na takwimu za matumizi kwa ufuatliaji na kujifunza zaidi hapa.

 

Source: StatCounter Global Stats – OS Market Share

© 2024, WEBNERD SOLUTIONS