Jinsi ya kuitumia google kupata unachokihitaji kirahisi zaidi!

Habari,  tovuti hii www.google.com ni moja kati ya zana zangu muhimu sana tangu nianze kutumia wavuti(internet). Achilia mbali kutafuta mambo mbalimbali, pia napata hiduma nyingi sana ambazo nitakuwa nawaeleza kadri siku zinavyokwenda, kwa leo ningependa kuhusisha njia ninazozitumia mara kwa mara kupata ninachokitaka kirahisi zaidi.

1. kitufe cha leo ni siku yangu (i’m feeling luck)

Kitufe hiki hutumika endapo unataka kupata kitu fulani na kifunguliwe kabisa, mfano: fungua google, kisha andika “Tanzania” kisha bofya(click)  kitufe(button) hicho, hapo utapelekwa moja kwa moja kwenye ukurasa ambao google huhisi ndio hasa unaoutaka, mara nyingi ni ule ukurasa wa kwanza kupatakana kipindi inatafuta. Ni njia ndogo na unaweza usione umuhimu wake ila kama neno ulilotumia kutafuta uko na uhakika nalo basi utapata unachokitaka bila haja ya kuanza kujiuliza kama ambavyo utabofya kile kitufe kingine.

2. Tafuta kwa picha (Image Search)

Ilishawahi kusemwa kwamba picha hubeba maelezo mengi kuliko maandishi, ikiwa unataka kutafuta kitu na umefanya hivyo kwa njia ya kawaida na unapata shida kukibainisha, basi tumia huduma ya kutafuta kwa picha, maana utakacho kiona pengine ndicho na ukiibofya tu basi inakupeleka ulikokutaka bila shida. Mimi binafsi nilipotelewa na mtu(rafiki) kwa kipindi kirefu na nilitumia huduma hii nikampata mara moja, kwa picha zake alizowahi kuzirushia facebook. inasaidia sana ukitafuta kitu kwa picha!

Mbali na kutumia picha, pia unaweza kutafuta kwa kutumia Ramani(Maps), Habari(News), Maswali na Majibu (Q&A) na mengine mengi.

3. Tumia viunganisho kama & || “”

mfano unataka kutafuta dr. slaa, ukiandika hivyo google itakuletea kurasa zenye neo dr na zenye neno slaa ndani yake, hii inaweza kuwa haitoshi kwako na ikakujazia kurasa nyingi na pengize hakuna unyoitaka hata, basi andika hivi “dr. slaa”, hapo itakuletea kurasa zenye neno hilo kama lilivyo na pengine utapata ulichokitafuta vyema kabisa.

Ikitokea unataka  kupata kurasa zinazo muhusu dr slaa, chadema, n.k, basi fanya hivi: “dr. slaa” & “chadema” hapo utapata kurasa zenye neno dr slaa  na chadema, la! pengine unataka dr slaa au chadema basi andika hivi: “dr. slaa” || “Chadema” hapo utapata kurasa zenye neno dr.slaa au zenye chadema.  Viunganisho hivi vinafurahisha sana, mara nyingine unajua ukitafuta dr. slaa, basi kurasa zitakazokuja kwa vyovyote vile zitakuwa na chadema, lakini hutaki hivyo pengine umeshaziona zote, na hamna utakacho, ila bado unataka kupata zenye dr. slaa bila chadema au zenye chadema bila dr. slaa, basi andika hivi: “dr. slaa” XOR “chadema”hapo google itakuletea zenye kimoja kati ya hivyo lakini si zenye vyote tofauti na hapo, italeta kurasa chache sana (raha!).

NB: & = AND, || = OR, nimetumia dr slaa na chadema kama mfano, ni vigumu sana kupata dr slaa bila chadema katika ulimwengu  huu tuliopo sasa!

4. ufafanuzi ( definitions)

Kipindi niko chuoni, google ilinisaidia kufahamu vitu vingi sana kirahisi. Tuseme nataka kujua chakula(food) ni nini?, basi huwa naandika hivi:-define:food, hapo google itaniletea fafanuzi(definitions) kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kwa kifupi ambapo nikipata moja inayonipendeza naweza kufungua tovuti yake nikajifunza zaidi, maisha yalikuwa rahisi sana kwangu, si unajua walimu wengine huwa wana-complicate hizi definitions, pale utapata ambazo ni rahisi na za kueleweka mno.

hii huwa bora zaidi kama unatafuta kwa kiingereza na kuna maneno mengi unaweza kupachikia kabla ya mkato mkuu(full colon) kama about, where, index of, n.k.. kama define linavyotumika.

5. Tafuta kwa aina ya faili kama (pdf, chm, mp3, wav)

kuna wengine huwa watafuta kitu bila kubainisha ni aina gani ya kitu anatafuta, mtafuta vitabu anaweza akapata vitabu kirahisi kama atandika jina la kitabu kisha mabano ndani akaweka extension ya kitabu anachikitafuta mfano: food and drinks book ( pdf || chm), hapo utaletewa kurasa zenye vitabu au viungo vya kitabu vya kusomeka kwa Adobe reader (pdf) au vile vya windows help viwer (chm).

Bila shaka nitakuwa nimehusisha mojawapo ya njia zinazonifurahisha na kunisaidia sana ninapotumia wavuti kwa kujifunza, kujitaarifu,kujiburudisha pia. Zijaribu njia hizi kama hukuwahi kuzifahamu hapo awali, na endelea kupitia tovuti hii kwa kujifunza mambo mengine mengi zaidi.

© 2024, WEBNERD SOLUTIONS