VIDEO: Tumia Windows kwa Kiswahili

Habari, Je!, wewe ni mpenzi wa lugha ya kiswahili?, na ungependa kutumia kompyuta yako au kifaa cha cha windows kikiwa na lugha hiyo?. Mikrosoft windows ana kifurushi cha lugha yetu pendwa na kinaweza kutumika kwenye kompyuta yako.

Kwenye makala hii nitakuonyesha namna unaweza kufanya kompyuta yako yenye Windows 8 ambayo pia inafanana na baadhi ya vifaa vya Windows Mobile iwe kwa lugha ya kiswahili, na hata lugha nyingine pia kama utapenda, namna ya kufanya hivyo hakutofautiani sana.

Utahitaji kuwa mtandaoni na kifaa chako, ili uweze kupakua kabrasha la lugha, ba baada ya kuingiza lugha kama utakavyoona, itabidi utoke (sign out/logout) na uingie tena(sign in/login) ili kuona mabadiliko ya lugha kwenye kifaa chako.

Angalia video hii hapa chini kujifunza.

Jinsi ya kusanikisha Movie Maker kwenye Windows 8

Habari wadau, ni muda sasa umekwenda lakini si mbaya leo tukijifunza kitu pia. Umewahi kujiuliza Video zinafanyiwa vipi editing?. Kama ndio bila shaka umeshafahamu kuwa Editing inafanyika zaidi kwenye Computer, na kuna programs au software ambazo nyingi ni ghali kuzinunua ambazo zitakuwezesha kufanya jambo hilo.

Kabla hatujazifahamu programu zinazotumika kwa shughuli hiyo, kwanza tujifahamishe kuhusu sifa zake za msingi. Programu ya Editing inategemewa kukuwezesha mtumiaji kufanya mambo yafuatayo:

  • Kuweza kufanyia kazi aina tofauti za mafaili utakayokuwa nayo, na kuweza kuyabadili mafaili hayo kwenda kwenye mfumo mwingine; aina za mafaili ni kama avi,mp4,mpg,jpg png,mp3 n.k
  • Kuunganisha vipande vya video, kukata sehemeu za video ambazo hutaki ziwepo na kuziondoa,
  • Kufanya angalau baadhi ya marekebisho kwenye sauti ya video ikiwa ni pamoja na kuongeza sauti ya ziada kama voice-over, athari za sauti na muziki wa nyuma kwenye video hiyo
  • Kufanya angalau marekebisho ya muonekano wa video husika, kama vile mwanga n.k, hapa tunazunguzia filters na effects mbalimbali ambazo zitapendezesha video yako machoni kwa watazamaji.
  • Kuwa na uwezo wa kuongeza mabadiliko kati ya sehemu za video zilizo katika mtiririko wa hadithi mfano picha kufifia, kupunguzwa, unafifia na nyeusi, unafifia na nyeupe n.k.
  • Kuwa na uwezo wa kuongeza maneno na vijimaneno kwa udhibiti mzuri na makala aina mbalimbali kwa ubunifu.

Hizi ni sifa za msingi kuwa nazo katika programu ya kurekeishia video zako. Hivyo kama una kamera nzuri inayoweza kurekodi video safi na una kompyuta nyumbani bila shaka utatamani kutumia programu hizi ili kupunguza gharama, maana waweza rekebisha video zako na kuzichoma kwenye CD na ukahifadhi kumbukumbu zako kisasa zaidi, au sio?.

Kwa ujumla ziko programu nyingi maarufu, na kama nilivyokwisha bainisha awali ni kuwa nyingi kati ya hizo zinauzwa na zina mambo mengi ya ziada ambayo si ya lazima sana kuwa nayo kwa video zako za nyumbani, hivyo Microsoft Windows huwa inawapatia watumiaji wake programu ambayo ni bure na inakuwezesha kufanya yote ya msingi.

Programu hii inaitwa Windows Movie Maker na kwa bahati mbaya inaweza isiwepo kwenye baadhi ya kompyuta zenye programu endeshi ya windows. Kama haipo kwenye kompyuta yako pia nenda hapa kuipakua kulingana na toleo la Windows yako. Utaipakua na kisha kuisanikisha kwa kufuata maelekezo yake.

Ukiifungua programu hiyo itaonekana hivi:

mm

Movie Maker Ikifunguka

Ni matumaini yangu utaweza kujifunza zaidi jinsi ya kuitumia programu hiyo kwa iko rahisi na vitu vyake viko wazi sana kuielewa, na pengine waweza kuja kuwa editor mzuri zaidi hata ukapata hamu ya kutumi programu kubwa za aina hii.

Endelea kufurahia kompyuta yako.

© 2024, WEBNERD SOLUTIONS