+255 717 074797   bbk@webnerdtz.com

Tumia program za Windows kwenye Linux!

Linux ni moja kati ya mifumo mashuhuri ya uendeshaji kompyuta, imekua ikitumika tangu miaka ya 1984. Programu hii hupatikana bure kabisa na katika ladha tofauti zinazofahamika kama ditros, kati ya distro maarufu sana duniani ni Ubuntu, Linux Mint, na fedora. Tofauti na Windows au Mac za Apple, kwenye Linux programu zote waweza pata bure pia […]

Linux ni moja kati ya mifumo mashuhuri ya uendeshaji kompyuta, imekua ikitumika tangu miaka ya 1984. Programu hii hupatikana bure kabisa na katika ladha tofauti zinazofahamika kama ditros, kati ya distro maarufu sana duniani ni Ubuntu, Linux Mint, na fedora. Tofauti na Windows au Mac za Apple, kwenye Linux programu zote waweza pata bure pia bila gharama yoyote.

Ingawa ni ya bure, Umaarufu wa Linux pia hutokana na uwezo wake wakutosumbuliwa na virusi (Computer Viruses) kama ilivyo kwenye Microsoft Windows, na uwezekano wa kupata msaada kwenye mtandao kwa urahisi na haraka sana.

Changamoto kubwa kwa wanaoanza ama kuhamia kutoka kwenye Windows na kuanza kutumia Linux, hasa Ubuntu, huwa ni kuzoea muonekano, na zaidi ni kupata programu (Softwares) ambazo alikuwa anazitumia kwenye Windows. Mfano, programu ya Kuchapa (Microsoft Word) na nyinginezo nyingi. Kwenye Linux kuna programu Mbadala ya zile zilizoko kwenye Windows, hata hivyo zinaweza zisifikie kiwango na ubora wa zile za kwenye Windows, lakini kwa kiasi kikubwa zinaweza kukusaidia kufanya unayohitaji kama ambayo ungefanya kwenye windows. Mifano ya programu mbadala zilizoko tayari ndani ya ubuntu ni kama ifuatavyo:-

  • Mozilla Firefox – kuperuzi wavuti, waweza pia kuingiza google chrome
  • Libre Office – mbadala wa Microsoft Office
  • Mozilla Thunderbird – mbadala wa Microsoft Outlook
  • Document Viewer – Mbadala wa Adobe reader
  • Rythimbox Music Player
  • Videos Media Player

 

Nitazungumzia namna mbalimbali ambazo unaweza kuzitumia kwenye linux kufanya kama ambavyo unhgefanya kwenye windows. Njia hizi baadhi zaweza kukusaidia pia hata ikitokea umeenda sehemu na ukakuta kompyuta inatumia mifumo wa linux badala ya windows uliyozoea mfano kwenye Internet Cafe.

1 : Tafuta mbadala wa programu.

Kuna tovuti maarufu sana inaitwa osalt.com, tovuti hii inakuonyesha programu mbadala wa programu nyingi ambazo zinauzwa. Mibadala hii si kwa ajili ya Linux/Ubuntu peke yake, yaweza pia kutumia kwenye Windows, Mfano Ukitaka mbadala wa Microsoft Word, utakuta kuna nyingi ikiwemo, AbiWord, OpenOffice Writer, KWord n.k.

2 : Tumia programu za online

Siku hizi kumeibuka teknolojia ya Cloud Computing ambayo inawezesha mtumiaji wa kumpyuta kutojali kuwa na kifaa fulani tu ili kuona na kufanya kazi zake. Cloud Computing inasaidia pia kushirikiana na wenzako na huna haja ya kubeba kompyuta tena kama unasafiri, ili mradi unakoenda kuwe na kompyuta na mtandao. Hivyo kuna huduma nyingi mtandaoni zinazowezesha wewe kuhifadhi mafaili yako ikiwemo nyaraka, picha, miziki na hata video na ukaweza kuvipata katika vifaa vingi tofauti.

Kwa njia hii unaweza kutumia linux na ukiwa na mtandao basi utachapa barua zako ikiwa online, baadhi ya huduma za bure unazoweza kutumia ni kama:-

  1. Google Drive kuhifadhi mafaili na Google Docs kama mbadala wa Microsoft Office
  2. Drop Box kuhifadhi mafaili yako ya aina zote.
  3. Office Online hii ndio kila kitu kama cha Microsoft Office ila ni online
  4. PIXLR hii ni kwa wale wanotumia photoshop na programu za graphics.

 

Kwa kila ain aya programu, ina mpbadala wake kwenye wovuti, hivyo ni wewe kutafuta tu.

3 : Sanikisha programu kwa kutumia WINE au PlayOnLinux.

Kuna programu inaitwa WINE ikimaanisha “Wine is not Emulator” ambayo inakuwezesha kusanikisha(Install) programu za Windows moja kwa moja kama vile iko kwenye Windows. Programu hii unaweza kuitafuta ndani ya Ubuntu kwa jina la Wine au PlayOnLinux. Ukishakuwa nayo unaweza kusanikisha baadhi ya programu muhimu kama Microsoft Office, Adobe Photoshop, na nyininezo nyingi.

4 : Sanikisha Windows kwenye Virtual Machine

Kwa kuwa Linux/Ubuntu inahakikisha usalama zaidi dhidi ya virusi vya kompyuta, na iko haraka kuliko Windows, unaweza pia ukaingiza Windows ndani ya Ubuntu kwa kutumia programu maalumu inayoitwa Virtual Box. Virtual Box inaweza kutengeza mfano wa kompyuta nyingine (Virtual Machine) ndani ya kompyuta yako uliyonayo, halafu ukaingiza windows na ukatumia programu zako unazotaka endapo njia nilizoordhesha hapo juu hazikufaa.

ZINGATIA: Hatua hii ya kutumia Virtual Box waweza pia kuifanya ndani ya Windows na ukasanikisha ubuntu ili kuijaribu na kujifunza kabla haujaamua kuitumia rasmi.

Bila shaka umeweza kupata angalau uelewa wa namya kutumia baadhi ya programu uzipendazo kwenye Windows ndani ya Linux. Kwa maoni, maswali na ama ushauri usisite kuniandikia kwenye fomu ya maoni hapo chini, ama kutuma ujumbe wako kwenda info@webnerdtz.com

Comments are closed.